24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KCMC kujenga maabara ya corona

Safina Sarwatt – Moshi

HOSPITALI ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC), imesema iko kwenye mchakato wa hatua za kuanzisha maabara ya virusi vya korona ili kukabiliana na vizusi hivyo endapo itabainika kuwepo kwa mgonjwa wa korona. 

Mkurugenzi wa Mtendaji wa KCMC na Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaria Mwema la Tanzania, Professa  Gilearrd Masenga aliyesema hayo jana, wakati wa ibada ya shukrani ya maadhimisho miaka 49 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo kuelekea miaka 50 .

Professa Masenga, alisema hospitali tayari imetenga eneo maalumu kwa ajili kujenga maabara ya virusi vya korona. 

Alisema hospitali imejipanga kwa vifaa tiba pamoja na watalaamu kwa ajili ya dharura, endapo itatokea mgonjwa mwenye virusi vya korona kwa kushirikiana timu ya mkoa. 

“Tumejipanga kwa vifaa na watalaamu wetu wako tayari muda wote,tunashirikiana na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi  na timu iliyondwa na ofisi ya mkuu wa mkoa, nawaondoa hofu wananchi kwamba tupo vizuri, “alisema professa Masenga. 

Alisemakutokana na mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa ambayo inapokea wageni wengi kutoka nje ya nchi kwa sababu za utalii wa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, umeimarisha huduma muda wote.

Alisema  hospitali hiyo, ina madaktari na wauguzi wa ngazi mbalimbali, madaktari bingwa 76 ,madaktari wa kawaida 74 na madaktari wasaidizi wanne  na (Clinical officers) 6.

Alisema kwa miaka 49, sasa kuelekea jubilee ya miaka 50 ,hospitali   imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika fani ya kitabibu kwa kanda nzima ya kaskazini pamoja na taifa. 

“Mafanikio haya yanatokana na jitihada za uongozi na  watumishi vitengo mbalimbali ndani ya hospitali ambao wamekuwa uti wa mgongo katika hatua tunazopiga siku baada ya siku, “alisema. 

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo aliipongeza hospitali hiyo kwa hatua kubwa waliyopiga katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi, ambapo aliwataka kuongeza juhudi zaidi  ili kuhakikisha kwamba wanaondoa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles