26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kaya 25,446 zaondolewa TASAF

simbachaweneNA AZIZA MASOUD, DODOMA
SERIKALI imeziondoa kaya 25,446 zisizo na sifa ya kuingia katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Tasaf) kati ya milioni I.I zilizoandikishwa katika halmashauri 159 nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene  wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Sabreena Sungura (Chadema).

Sungura alihoji Serikali imejipanga vipi kutatua kero kwa wananchi ambao hawapati fedha hizo, hususani katika Mkoa wa Kigoma.

Simbachawene alisema kaya hizo zimetolewa baada ya kufanya mapitio ya orodha na ukaguzi wa nyumba kwa nyumba katika wilaya zote za Tanzania Bara pamoja na Unguja na Pemba hadi kufikia Mei 30, mwaka huu.

Alisema watu walioondolewa katika orodha hiyo ni pamoja na wajumbe wa kamati za mpango (CMC), viongozi wa vijiji, mitaa na shehia, vifo pamoja na baadhi ya kaya  kukosa vigezo vya umaskini.

Simbachawene alisema mpango huo ni endelevu kwa kuwa baadhi ya jamii na viongozi walifanya udanganyifu kwa makusudi  na kuingiza majina ya kaya ambazo si maskini sana na kuziacha kaya zinazostahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles