33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mkuu Tamisemi awakumbusha wakurugenzi

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

KATIBU Mkuu Tamisemi, Joseph Nyamhanga, amewataka wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuhakikisha hoja zote zilizoibuliwa kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zinajibiwa na kuyafanyia kazi mapendekezo ya wakaguzi kwa kuanzia na wakaguzi wa ndani.

Nyamhanga alitoa kauli hiyo jana jijini hapa wakati akizungumza  kwenye kikao kazi cha upokeaji na uhakiki wa taarifa za majibu na mipango kazi ya utekelezaji wa hoja na mapendekezo ya CAG kwa hesabu za mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2017/18 .

Alisema kwamba, ni muhimu hoja zote zifanyiwe kazi haraka na kwa ufasaha ili kunusuru upotevu wa fedha na kuboresha utendaji na kuimarisha utawala bora, jambo ambalo ndio msingi wa ukaguzi.

“Tukifanya hivyo, hoja zisizo za lazima zitaondoka na hata wakaguzi hawatatumia muda mwingi katika kufuatilia mambo ya msingi zaidi katika kuboresha utendaji.

“Katika kujibu hoja za CAG na kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa maagizo ya CAG ya hesabu za mwaka 2016/17, imeonekana kufikia Januari 2019, jumla ya hoja asilimia 47 zilifungwa na asilimia 53 zilikuwa bado hazijajibiwa,” alisema Nyamhanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Miriam Mmbaga, alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwawezesha watendaji hao kujibu hoja za CAG na kuongeza uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili hoja hizo zisijitokeze tena katika halmashauri zao.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, alisema kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri, kuwa halmashauri zimekuwa zikikabiliana na changamoto mbalimbali katika kujibu hoja za ukaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles