25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KATIBU MKUU MADINI AHIMIZA UWAJIBIKAJI

Na VERONICA SIMBA -DODOMA

KATIBU Mkuu mpya wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, amewataka watumishi wa Wizara kuwajibika katika nafasi zao ili wananchi wanufaike na matunda ya kazi ipasavyo.

Profesa Msanjila aliyasema hayo juzi baada ya kuwasili rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma na kupata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi.

Alifafanua kuwa, uwajibikaji hupimwa kwa matokeo. “Tutakuuliza umefanya nini katika nafasi yako ili tuweze kupima utendaji wako,” alisema.

Profesa Msanjila alisisitiza ushirikiano baina ya viongozi na wafanyakazi wote ili kupata matokeo chanya, hivyo kuleta manufaa katika sekta ya madini.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, aliahidi ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi na uwajibikaji katika nafasi zao kama alivyoasa Katibu Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles