30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu CCM ampiga kombora Wenje

wenjetaNA PETER FABIAN, MWANZA

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, amewataka wananchi wa Jimbo la Nyamagana wamhoji Mbunge wa Jimbo hilo, Ezekiel Wenje, jinsi fedha za mfuko wa jimbo lao zilivyotumika kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Mtaturu alisema hayo juzi jijini Mwanza kwa nyakati tofauti, wakati akihutubia wakazi wa Bugarika, Kata ya Pamba na alipokuwa akizindua shina la vijana waendesha pikipiki ambao ni wafuasi wa CCM katika Mtaa wa Nyamagana Magharibi.

“Fedha za mfuko wa jimbo hutolewa na Serikali ya CCM kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya jimbo, lakini mwenyekiti wa mfuko ambaye ni mbunge wenu, amekuwa akizitumia kwa kazi tofauti.

“Kwa hiyo umefika wakati wananchi mumhoji mbunge wenu ili awape majibu ya kueleweka na asiendelee kuwapa viroba vya pombe na kuwatukana viongozi wa Serikali na CCM.

“Kazi ya mfuko huo ni kuchochea maendeleo kwenye jimbo, lakini fedha hizo jimboni kwenu hazijafanya kitu, ingawa mwaka 2014/2015 zilitumika kununulia mifuko 80 ya saruji kwenye shule kadhaa za msingi baada ya madiwani wa CCM kuingia kwenye kamati ya mfuko huo.

“Pamoja na kwamba hajaleta maendeleo, Wenje amekuwa akijinadi kwenye mikutano ya hadhara kuwa amefanya kazi na kuwaletea maendeleo wananchi wa Nyamagana, lakini maendeleo hayo hayaonekani machoni.

“Kwa hiyo ndugu zangu wananchi, muda wa uchaguzi ukifika ni vema mkamtosa Wenje na kumchagua mtu sahihi kutoka CCM badala ya kuendelea kuwa na mbunge mtalii kama yeye,” alisema Mtaturu.

Awali akizindua tawi la vijana hao, Mtaturu aliwataka waige mfano wa waendesha bodaboda waliojiunga kwenye vikundi kwa ajili ya kuwezeshwa na Serikali.

Pia, aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi wakati wa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura ili wapate fursa ya kuchagua viongozi bora kutoka CCM.

Pamoja na hayo, Mtaturu alipokuwa Bugarika, alimuagiza Ofisa Mtendaji wa Kata ya Pamba, Charles Musso, aondoe dampo la taka lililorundikana katika makazi ya wananchi wa eneo hilo kwa kuwa linaweza kusababisha magonjwa ya milipuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles