24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kasi ya ubakaji yawashtua viongozi wa dini

Mwandishi wetu

Ongezeko la matukio ya ubakaji nchini limewashtua viongozi wa dini na kusababisha baraza la mahusiano ya dini mbalimbali kwa ajili ya amani nchini kutoa wito kwa viongozi hao kuamka usingizini na kukemea vitendo hivyo ikiwamo ndoa za utotoni.

Kauli hiyo imekuja kutokana na ongezeko la matukio ya ubakaji kwa wasichana kuzidi kuongezeka ambapo kwa mujibu wa takwimu zilizoripotiwa katika vituo vya polisi, zaidi ya wasichana 22,000 wamebakwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2017.

Akizungumza katika warsha ya viongozi wa dini nchini iliyoandaliwa na Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni (TECMN), Mwanasheria kutoka katika mtandao huo, Fundikira Wazambi amesema takwimu hizo zinaonesha kwa mwaka wasichana 4,500 wanabakwa.

Naye Katibu wa baraza hilo ambaye ni Paroko wa Parokia Magomeni, Likoko Nyumayo amesema tatizo ni mavazi ambapo amelitaja kama tatizo ambalo limekuwa likiongezeka kila kukicha jambo ambalo linadhihirisha jamii inazidi kupotoka.

Aidha, Mchungaji Erika Ludela alisema kina mama wanatia aibu kutokana na kuwavalisha watoto wadogo wa kike vimini ambavyo hata jamii inayowazunguka inawashangaa.

“Niliwaita wazazi wa jinsia zote mbili, akina baba na mama, kwa kweli akina baba walikiri kuwa akina mama wanawanunulia na kuwavalisha watoto vinguo vinavyowabana.

“Haya ni mambo ya kuiga ambayo hayana maadili kwa jamii zetu, lazima kina mama wabadilike, mimi ni mwanamke ila ninakerwa sana kuona watoto wadogo kabisa wamevalishwa vinguo vya ajabu na mwisho wa siku wakiwa wasichana wanaendeleza tabia hiyo na kuchochea matendo ya ngono,” alisema.

Kwa upande wake Imamu wa Msikiti wa Magomeni, Mursalina Mavere alisema kutokana na hali hiyo, umefika wakati sasa kwa serikali kuandaa sheria ambayo itakataza kabisa uvaaji wa mavazi ya aina hiyo yasiyo na stara.

“Kwa sababu ni jambo la aibu unapita mtaani unakutana na watoto, wasichana na wanawake wakubwa ambao wamevaa mavazi ambayo yanaamsha ashki za wanaume, sasa si wote wenye hofu ya Mungu, wengine ndiyo hao wanazidiwa na kubaka,” alisema.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao huo, kutoka Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Michael Jackson alisema mtandao huo umedhamiria kuwatumi viongozi wa dini kushirikiana na jamii kutokomeza ndoa za utotoni.

“Ili kufikia Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025, ni wajibu wa jamii kwa ujumla kuachana na mila hatarishi kama ukeketaji, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia, mambo yanayochangia kukandamizwa, na kurudisha nyuma maendenel ya mtoto wa kike,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles