24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KARIAKOO DERBY… JEURI YA SIMBA HII HAPA

NA WINFRIDA MTOI

ZIMEBAKI saa chache kabla ya mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kwenye Dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam kesho.

Kwa sasa hakuna habari nyingine ya soka mjini iliyoshika chati zaidi ya mpambano huo unaovuta hisia za wadau wa michezo, hasa mashabiki wa timu hizo mbili wanaotambiana kila kona.

Kuelekea mchezo huo, mashabiki wanaoonekana kujiamini zaidi ni wale wa Simba, tofauti na wenzao wa Yanga ambao wanazungumza kwa hofu kutokana na baadhi yao kutoamini ubora wa kikosi chao.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 24 kutokana na mechi 11, ikishinda saba, sare tatu na kupoteza moja.

Kwa upande wao, Simba ipo kileleni na pointi 34, ilizovuna ndani ya mechi 13, ikishinda 11, sare moja na kupoteza moja.

Kukaa kileleni kwa muda mrefu ni moja ya sababu inayowafanya Wanasimba kujiamini zaidi lakini pia kukiwa na mengine yanayochangia hilo.

C.E. O Senzo

Tangu kutua kwa Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa klabu hivyo, Senzo Mazingiza, Simba imekuwa na mabadiliko makubwa hasa katika utendaji kuanzia benchi la ufundi, wachezaji na hadi uongozi. 

Senzo ameingia na kasi ya aina yake, akiwa hataki masikhara katika kazi, huku pia akiwa karibu na timu pamoja na mashabiki wa kikosi hicho, akionekana uwanjani mara kwa mara akitoa kauli za ushindi. 

Pia, uwezo na wasifu wake kutokana na klabu alizopitia, unawaaminisha Wanasimba kuwa hakuna wakuwalinganisha nao kwa sasa.

Ubora wa kikosi

Hakuna ubishi, Simba ina kikosi kipana na chenye wachezaji wenye viwango vizuri ukilinganisha na timu nyingine za Ligi Kuu Tanzania.

Katika kikosi cha Simba, hata kukiwa na majeruhi, hakuna hofu kuwa watashindwa kucheza mechi na kupata matokeo mazuri kwa sababu wana mchezaji zaidi ya mmoja katika kila nafasi.

Mfano mzuri ni katika mechi nne za hivi karibuni ambapo Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sven Vanderbroeck, ameonekana kupanga vikosi vitatu tofauti kuanzia mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam, ambao ulikuwa mchezo wake wa kwanza.

Kasi ya Deo Kanda

Winga huyo raia wa DR Congo, kiwango chake kimezidi kupanda tofauti na mechi za nyuma, akitengeneza na kufunga mabao.

Sven kama ndiye amekuwa mganga wake, kwani tangu ameanza kukinoa kikosi hicho, kiwango cha Kanda kimebadilika na kuwavutia wapenzi wengi wa timu hiyo, hivyo kuwapa jeuri kuwa hata katika mechi ya watani kesho, ataendeleza moto wake.

Kurejea kwa John Bocco

Straika huyo mkali wa mabao, alikosekana uwanjani kwa muda mrefu, tangu alipoumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, uliopigwa Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa.

Bocco ameanza rasmi kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Ndanda FC, walioibuka na ushindi wa mabao 2-0. Licha ya kushindwa kufunda lakini alionekana alifanya majaribio ya hapa na pale. 

Kumiliki uwanja

Wekundu wa Msimbazi hao kwa sasa hawana tena ile changamoto ya kutafuta ni uwanja gani mzuri wanaweza kujificha kujiandaa na mchezo huo kwa sababu wana wa kwao na wanaamua wenyewe ni muda gani wafanye mazoezi.

Simba inatumia viwanja vyao vya Mo Simba Arena, vilivyopo Bunju, jijini Dar es Salaam, ambao wanaamua watumie wa nyasi bandia au kawaida, tofauti na watani zao.

Sakata la kuondoka wachezaji Yanga 

Kitendo cha baadhi ya wachezaji wa Yanga kuamua kuachana na timu hiyo, kinachangia Simba kuwa kifua mbele kwa kuwa wanaamini wale waliosajiliwa kuziba mapendo bado hawana uhakika kama wataendana na mchezo huo kutokana na kukaa muda mfupi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles