28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KARDINALI PENGO: NAELEKEA KUCHOKA

SALAMU: Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akisalimiana na waumini wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya kumpokea msaidizi wake Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi (kulia), iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam juzi.

Na AGATHA CHARLES


ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema alimwomba Kiongozi wa kanisa hilo duniani Papa Francis  kumpatia msaidizi kwa kuwa anaelekea kuchoka.

Kardinali Pengo alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati wa ibada ya misa Takatifu ya kumpokea msaidizi wake huyo ambaye ni Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam.

Kardinali Pengo alisema ingawa hakupendekeza jina la ni nani apatiwe lakini anamshukuru Mungu kwa kumpatia Askofu Ruwa’ichi.

“Ni mimi niliyeomba kwa Baba Mtakatifu anipatie mwandamizi na sikutaja jina.  Namshukuru Mungu ombi langu limekubaliwa.

“Askofu Ruwa’ichi ulikuwa na nafasi ya kusema hapana wala usingepewa adhabu. Anayeomba msaada kama wangu maana yake anaelekea kuchoka,” alisema Askofu Pengo.

Kardinali Pengo alimweleza Askofu Mkuu Mwandamizi Ruwa’ichi kuwa bado wana nafasi ya kuzungumza  mengi zaidi hadi pale Mungu atakapoamua tofauti.

Zaidi Kardinali Pengo alisema hata kama atakabidhi kazi kwa Askofu Mkuu Mwandamizi lakini hataweza kuishi nje ya Dar es Salaam kwa kuwa ni eneo alilozoea na amefanya kazi ya utume kwa miaka 28.

“Ila hata kama nitakabidhi kazi kwa Baba Askofu sitatoka …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles