29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za bima zatakiwa kutoa elimu umuhimu wa bima

Na Susan Uhinga, Tanga



Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amezitaka taasisi za bima nchini kutafuta njia rafiki ya utoajia elimu wa umma ili waweze kuwafikia wananchi wote wakiwamo, wakulima na wafugaji kwa lengo la  kuwapatia elimu sahihi na faida ya kuwa na bima.

Waziri Mpango ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 21 wa bima ulioandaliwa na taasisi ya umoja wa  makampuni ya Bima uliofanyika mkoani Tanga.

Amesema Watanzania wengi hawana utaratibu wa kujikatia bima, sababu kubwa ni ukosefu wa elimu kuhusiana na umuhimu wa bima hivyo ameagiza taasisi za bima kuweka mpango rafiki wa elimu utakaowafikia Watanzania wote.

“Kuwa na bima ni muhimu kwa kuwa inasaidia kutukinga na majanga yanayoweza kutokea wakati wowote kama mlivyoona kwa Watanzania waliopoteza maisha katika ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere, hawakuwa na bima jambo lililosababisha Rais John Magufuli kuona huruma na kutoa Sh milioni moja kwa kila marehemu,” amesema.

Aidha, amezitaka taasisi hizo kumpelekea mapendekezo ya maboresho ya sera ili serikali iweze kuyafanyia kazi kwa manufaa ya Watanzania.

Kwa upande wake Kamishna wa Bima nchini Dk. Baghayo Saqware ameeleza mikakati yao kwa mwaka 2018 hadi 2020  kwamba wamejipanga zaidi kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu kuanzia ngazi za mitaa pamoja na wajasiriamali wadogo.

Katika hatua nyingine, taasisi hiyo ya bima nchini imekabidhi rambirambi ya Sh milioni 20 kwa Serikali kwa ajili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles