23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kamishna Mhifadhi wa Misitu awasili ofisini kwake

Na Loveness Bernard, Dar es Salaam

Kamishna Mhifadhi wa Misitu, Profesa Dos Santos Silayo amewasili ofisini kwake zilipo ofisi za makao Makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), zizilizopo jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza tangu avikwe cheo hicho

Profesa Silayo alivikwa cheo hicho na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dk. Hamisi Kigwangalla, Julai 9 mwaka huu katika sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato  zilizofanyika wilayani Chato mkoani Geita ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuwasili ofisini hapo na kupokelewa na viongozi waandamizi na watumishi wa TFS, leo Julai 12, Profesa Silayo amesema mabadiliko yanayotokea katika sekta ya maliasili yamepelekea pia kubadili mfumo wa usimamizi na utendaji wetu toka ule wa kiraia kwenda Jeshi Usu.

“Namshukuru Mungu kuwa sehemu ya mabadiliko hayo, hatua hiyo ikapelekea kuvikwa cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na Waziri Kigwangala, mabadiliko haya yanalenga kujenga uwezo wa taasisi, uwezo wa watumishi ikiwa ni pamoja na kuwajengea ari, uzalendo, weledi na ujasiri katika kusimamia rasilimali za misitu na nyuki.

“Natoa shukurani kwa Rais Magufuli na viongozi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo waliyofikia ambayo anaamini itasaidia kukuwa kwa sekta ya misitu nchini na kuongeza ushirikiano na wadau wengine hususani wananchi katika kusimamia misitu yetu,” amesema.

 Aidha Profesa Silayo amesema uwezo wa watumishi wa TFS utaenda sambamba na weledi katika matumizi ya mbinu na vifaa vya kisasa vinavyoweza kumudu mabadiliko ya changamoto za uhifadhi kuanzia usalama wao pamoja na  usalama wa mali zenyewe unaotokana na kuongezeka kwa mbinu za kihalifu kila wakati.

Akizungumza kwa njia ya simu Naibu Kamishna wa Huduma Saidizi, Emmanuel Wilfred, amesema mabadiliko hayo yamepelekea kubadili mfumo wa usimamizi na utendaji wa TFS toka ule wa Kiraia kwenda Jeshi Usu na hivyo kulazimu watumishi wote kwenda kwenye mafunzo.

“Tunaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wachache waliobaki na kwa wale waliokwishakwenda kwenye mafunzo tunakamilisha taratibu ili Kamishna aweze kuwatunuku vyeo vyao, lakini niwatake wafanyakazi wote kuenda sambamba na mabadiliko kwa kasi hitajika,” amesema Wilfred.

Kwa upande wake mmoja wa watumishi wa TFS , Rosemary Sabida, amesema mabadiliko hayo yatawasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi nchini.

Kamishna Mhifadhi wa Misitu, Profesa Dos Santos Silayo akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) alipowasili katika makao makuu ya wakala hiyo jijini Dar es Salaam leo Julai 12.

Jumla ya Makamishna wanne, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dk. Allan Kijazi, Kamishna wa Uhifadhi wa Misitu toka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Silayo, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara na  Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk Freddy Manongi,  walivishwa vyeo vya kijeshi Julai 9, mwaka huu katika sherehe za Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato  zilizofanyika wilayani Chato mkoani Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles