25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati za Bunge kuchambua taarifa ya CAG

Mwandishi Wetu

Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza kuchambua taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hesabu za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni, mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa wa Ofisi ya Bunge, Kamati hizo 14 zitakazoketi vikao kuanzia Jumatatu Oktoba 21 hadi Novemba Mosi, mwaka huu, Jijini Dodoma pamoja na mambo mengine zitachambua taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma katika mashirika na taasisi mbalimbali nchini.

Aidha, zitapokea na kujadili Taarifa ya mapendekezo ya mwongozo wa kutayarisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya wizara na taasisi mbalimbali za serikali na kuchambua Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa mkutano wa 16 Bunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles