26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati Kuu CCM wakati wowote

Christopher ole SendekaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMATI Kuu ya Chama  Cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana wakato wowote kuanzia sasa    kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho.

Hata hivyo,  taarifa za ndani ziliiambia MTANZANIA kuwa katika hatua za awali tayari chama hicho kimepanga mkutano huo kufanyika  Julai 20 au 21 mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, alisema  kikao hicho ndicho kitaamua lini mkutano huo utafanyika.

Sendeka alisema ajenda kuu itakuwa ni kukabidhiwa chama kwa Rais Dk. John Magufuli kama ilivyo utamaduni wa chama hicho.

“Kikao cha CC ndicho chenye maamlaka ya juu na kitakutana wakati wowote na kupanga tarehe ya mkutano mkuu wa chama chetu,” alisema Sendeka.

Kikao cha mwisho cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kilikuwa  Februari 3, mwaka huu Ikulu ya Chamwino, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Katika kikao cha   Dodoma wajumbe  walishindwa kuafikiana tareehe ya mkutano mkuu jambo ambalo liliibua mjadala mzito hasa baada ya kuelezwa kuwa Rais  mstaafu Jakaya Kikwete hakuwa tayari   kukabidhi chama kwa kile alichodai hakuna fedha kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles