25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kama huoni vizuri usiku, kula tende kwa wingi

tende

Na Herieth Faustine,

Tende ni tunda linaloongoza kwa kuliwa katika kipindi cha mfungo wa Ramadhan kuliko matunda yote.

Tunda hili lina sukari nyingi… wakati mwingine huliwa zikiwa mbichi au zimeiva;.

Pamoja na kutumika zaidi katika kipindi cha mfungo pia lina ladha nzuri mdomoni, huku likisheheni madini na vitamini lukuki na hivyo kuwa na faida nyingi kiafya.

Tunda hili pia limethibitika kisayansi kuwa na madini ya aina nyingi pamoja na  vitamini lukuki ambayo yana faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Miongoni mwa faida za tende ni kusaidia kupata protini ya kutosha na vitamin B1,B2,B3,B5,A1 na C ambavyo ni muhimu katika mwili wa binadamu.

Pia husaidia kuupa mwili nguvu ili kuondokana na uchovu kutokana na tunda hili kuwa na sukari asilia (glucose). Ndiyo maana tunda hili hutumika zaidi wakati wa  mfungo wa Ramadhan ili kuupa mwili nguvu baada ya mfungo.

Vile vile ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo humsaidia mhusika kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo.

Hali kadhalika tende ina madini aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini hayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.

Pamoja na hayo tende pia huwasaidia wale wenye matatizo ya ugonjwa wa anemia, (kupungukiwa damu) wanapotumia tende huweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi.

Mbali na hayo inaelezwa kuwa matumizi ya mchanganyiko wa tende maalumu yaani maziwa, asali na unga wa hiriki huweza kuwa msaada kwa wale wenye shida ya nguvu za kiume.

Tende vile vile huimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles