24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

KAKOLANYA RASMI MWEKUNDU, MWEUPE

NA MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

NI rasmi kipa mahiri nchini , Beno  Kakolanya atavaa jezi zenye rangi nyekundu na nyeupe  kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba.


Kipa huyo amejiunga na  Wekundu hao, baada  ya  kuichezea Yanga kwa misimu minne, akitokea kikosi cha Maafande wa Jeshi la Magereza,Tanzania Prisons ya Mbeya.

Mwishoni mwa mwaka jana, Kakolanya aliomba kuvunja mkataba na Yanga, kutokana na kile alichodai klabu hiyo ilishindwa kumlipa shahiki zake, lakini hata alipopata ufumbuzi wa madai yake hakuweza kurejea katika kikosi hicho cha Jangwani, baada ya kuwekewa ngumu na kocha Mwinyi Zahera  aliyedai kipa huyo ni mtovu wa nidhamu.

Kusajiliwa kwake Simba, kumekamilisha tetesi za muda mrefu za kutakiwa na klabu hiyo ya Msimbazi, ambayo jana kupitia akaunti rasmi iliachia picha ya  kipa huyo akisaini  mkataba, akiwa na meneja wake, Selemani Haroub.

Horoub pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba.

Usajili wa  Kakolanya unafanya idadi ya wachezaji ambao mpaka sasa wamethibitika kumwaga  wingo wa kuichezea Simba msimu ujao kuwa watano.

Wengine ni kipa Aishi Manula,  John Bocco, Jonas Mkude  na  Erasto Nyoni ambao wameongeza  mikataba  ya miaka miwili miwili, baada ya awali kuelekea ukingoni.

 Kakolanya ni wazi atalazimika kupambana kweli kweli ili kupata nafasi ya kukaa langoni, kutokana na kukabiliwa na ushindani wa  Manula ambaye amekuwa akitumika kipa wa kwanza, akisaidiana na Deogratius Munishi ‘Dida’.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kakolanya alisema amesaini  Simba ili kupata ushindani ambao hakuwa anaupata kipindi akiwa Yanga.

“ Najua kuna ushindani wa namba na inaweza kuwa vigumu kumweka benchi Manula (Aishi), lakini nini naenda kufanya.

“ Yanga nilikuwa namba moja, sikuwa napata ushindani kitu ambacho kilinifanya nijione mimi ni bora, lakini uwepo wa Manula  Simba utanifanya niamini nitakuwa bora zaidi kwa kuwa nitalazimika kupambana zaidi ili nipate nafasi ya kucheza ,”alisema Kakolanya.

Mbali na Kakolanya, taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, zinaeleza kuwa aliyekuwa nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajib , pia amesaini kuichezea timu hiyo msimu ujao, ingawa hakuna uthibitisho uliotolewa na  klabu hiyo.

Wengine wanaotajwa sana ni pamoja na  straika wa Nkana ya Zambia,Walter Bwalya, ambaye yuko nchini tayari tangu juzi.

Pia Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ni kati ya walioongeza mkataba, huku Emmanuel Okwi akiwa mbioni kufanya hivyo.

Mtendaji wa Mkuu wa  Simba (CEO),Crescentius Magori, alisema, huo ni muendelezo wao wa kutambulisha wachezaji watakaoichezea timu hiyo msimu ujao.

“ Jana (juzi)nilisema  katika mkutano wangu na vyombo vya habari kuwa tumeshakamilisha usajili wetu kwa zaidi ya asilimi 90,  ikiwemo kuwaongeza mikataba  wachezaji wetu muhimu ambao kocha anawahitaji.

 “Usajili huu unalenga zaidi mashindano ya kimataifa yaliopo mbele yetu na ndio maana kila nafasi tunakuwa na wachezaji zaidi ya wawili.

“ Kila siku tutakuja na mtu mwingine, Wanasimba wasiwe na shaka tunafanya kazi kwa umakini mkubwa kwa kufuata matakwa ya kocha wetu ambaye ndiye mwenye jukumu la kuipa matokeo chanya timu,” alisema Magori.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles