31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kairuki ahimiza uwekezaji mikoani

Mwandishi Wetu-Songwe

WAZIRI wa Uwekezaji, Angela Kairuki ameziagiza mamlaka za mikoa kuhakikisha zinatekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuandaa maandiko yanayohusu fursa zanuwekezaji katika mikoa yao ndani ya muda uliowekwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji Mkoa wa Songwe jana, Kairuki alisema uongozi wa mkoa huo umeonesha kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kuandaa maandiko yanayoainisha fursa zote za uwezkezaji na namna ya kuzifikia, hatua ambayo inastahili pongezi.

“Naikumbusha mikoa ambayo bado haijaandaa makongamano hayo waharakishe kabla ya muda wa mwisho ulowekwa ili wakamilishe ndani ya wakati.

“Nia ya Serikali, ni kuhakikisha inawezesha ukuaji wa viwanda na kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025, kwa sekta ya kilimo ni muhimu kutekekeza na kufikia lengo hilo,” alisema.

Alisema kuna fursa nyingi mkoani Songwe, ambazo zinatokana na fursa za eneo la lango kuu la nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc), na ni vema kundelea kuwafahamisha wawekezaji njia sahihi za kuweza kuzifikia fursa hizo.

Alisema changamoto kubwa katika uwekezaji, imekuwa ni kuwa na maamndiko kuhusu maeneo gani yanayofaa na  namna gani ya kuyafikia na kwa hatua hii, imekuwa muhimu kwa kuweka wazi fursa zilizopo katika mkoa huo.

Alisema moja ya fursa waliyo nayo ni kilimo na kwa kuangalia uzalishaji wa kilimo wameshika nafasi ya kwanza kitaifa kwa uzalishaji msimu uliopita na wanaweza kuendelea kufanya vizuri katika sekta hiyo, hasa kilimo cha mahindi, mpunga na pareto.

Alisema ni kupitia kodi za wawekezaji hao na wanafanyabiashara ndipo Serikali inapopata mishahara kwa ajili ya wafanyakazi wake na kutoa huduma zote za jamii kwa watu wake, hivyo hao si watu wa kubezwa.

Alisema anatambua kuna changamoto ya kusafirisha mazao na bidhaa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia Zambia ambayo tayari wameanza kuzungumza na wenzao upande wa Zambia ili kuhakikisha changamoto hizo zinamalizwa.

Mwakilishi wa Jukwaa la Sekta Binafsi, (TPSF), Godfrey Simbeye alisema wanaona kinachotokea kwa wakati huu ni mabadiliko ya kifikra hasa katika suala la uwezeshaji wa wawekezaji ili kwenda na kasi ya mabadiliko yaliyopo.

“Lakini tunapensda serikali ijue kuwa watu ambao wanapitia utaratibu mrefu wenye usumbufu katika uwejkekezaji ni watu wa sekta binafsi na sasa hata viongozi wa Serikakli ndio wanacholalamikia,” alisema.

Mwakilishi wa EPZA, Nakadogo Phares alisema mkoani Songwe, mamlaka hiyo yenye jukumu la kuweka maeneo maalumu ya viwanda vya uzalishaji, kwa kuweka miundombinu yote inayowezesha mwekezaji kuweka viwanda, imeshirikiana nao zaidi kwa kuwangalia na kuwekaka mkakati wa namna bora ya kuinua mkoa huo katika uwekezaji.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema mkoa huo ni mchanga ila unastahili kupongezwa kwa kuwa ndani ya muda mfupi, tangu kutangazwa rasmi mwaka 2016, umeweza kushika nafasi ya kwanza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles