24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kagere na rekodi tamu ya mabao ya usiku

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KWA msimu wa pili sasa, nyota wa raia wa Rwanda, anayekipiga katika kikosi cha Simba, Meddie Kagere ameendelea kuwa moto kwa upachikaji wa  mabao Ligi  Kuu Tanzania Bara.

Kagere ambaye alijiunga na Simba akitokea Gor Mahia ya Ligi Kuu Kenya msimu wa 2018/19, amekuwa chaku  ya ushindi wa Simba kutokana mabao yake ambayo amekuwa akiifungia timu hiyo.

Katika msimu wake wa kwanza,  Kagere alimaliza ligi akifunga mabao 23 kati ya 77 yaliyofungwa na Simba ambayo ilifanikiwa kutwaa ubingwa.

Idadi hiyo ya mabao ilimwezesha kumaliza msimu akiwa mfungaji bora.

Mwenendo wa huo wa Kagere ni wazi amedhamiria kufuata nyayo za washambuliaji Amis Tambwe, aliyewahi kucheza Simba na Yanga kwa nyakati tofati na Simon Msuva, aliyekipiga Yanga kabla ya kutimkia Difaa Hassan El Jadida ya Ligi Kuu Morocco.

Tambwe na Msuva kila mmoja amewahi kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bpra wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo.

Msimu huu, Simba imeshuka dimbani mara 28 na kujikusanyia pointi 71, baada ya kushinda michezo 23, sare mbili na kuchapwa mara tatu.

Wekundu hao wamefanikiwa kupachika mabao 63 katika michezo hiyo 28, huku Kagere akifunga mabao 25 kati ya hayo na kutoa pasi tano zilizozaa mabao.

Achana na idadi ya mabao aliyoipa Simba hadi sasa, kitu kipya alichokifanya Kagere msimu huu ni aina ya mabao yake kwani mengi  kato ya hayo aliyafunga kipindi cha pili cha mchezo. Unaweza kuyaita mabao ya usiku.

Rekodi zinaonyesha kuwa, kati ya mabao 19 aliyofunga, 10 ameyafunga kipindi cha pili na tisa kipindi cha kwanza.

Bao la usiku zaidi ni lile alilofunga dakika ya 88 kwenye mchezo dhidi ya Namungo  ambao Simba ilishinda mabao 3-2, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao mengine tisa aliyofunga kipindi jua linaelekea kuzama ni dhidi ya JKT Tanzania,  mechi iliyoisha kwa Simba kushinda 3-1.

Katika mchezo huo Kagere akitupia moja dakika ya 58.

Pia mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao Simba ilishinda mabao 3-0 Uwanja wa Kaitaba.

Katika mchezo huo, Kagere alitupia mpira wavuni dakika ya 79.

Mechi nyingine ni dhidi ya Azam, iliyoisha kwa Wekundu hao kushinda 1-0, huku Kagere akiwa mfungaji dakika ya 48.

Katika mchezo dhidi ya Lipuli iliyoisha kwa Simba kushinda mabao 4-0, Mnyarwanda huyo aliweka mpira wavuni dakika ya 49.

Mechi dhidi ya Alliance, Simba ilishinda mabao 4-1, Kagere alifunga  bao dakika ya 58, lakini pia ule na Namungo ulioisha kwa vijana wa Mohamed Dewij ‘ MO’ walishinda mabao 3-2, akitupia dakika ya 88.

Katika mechi ya mzunguko wa pili kati ya Simba na Kagera,   bao la ushindi la Wekundu hao iliwekwa wavuni na Kagere dakika ya 61.

Mchezo dhidi ya Biashara United, Simba ilishinda mabao 3-1, Kagere alifunga dakika ya 68.

Mwingine ni mchezo dhidi ya Singida United, straika huyo alifunga bao dakika ya 70, wakati mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Azam iliyoisha kwa Simba kushinda mabao 3-2, mkali huyo alifunga dakika ya 71.

Kwa upande wa mabao ya mapema(mabao ya asubuhi), nikiwa na maana yaliyofungwa kipindi cha kwanza,, katika mechi 28 ilizocheza Simba, Kagere amefunga mara tisa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya JKT Tanzania, Simba ilishinda 3-1, Kagere alifunga dakika ya kwanza.

Simba na Mtibwa, Wekundi walishinda mabao  2-1, Kagere alitingisha nyavu dakika ya 17.

Mchezo mwingine ni ule wa Kagera , Simba ikishinda  3-0, Kagera alifunga dakika ya nne, ikicheza na Biashara na Simba kuibuka kidedea kwa mabao 2-0, Kagere alifunga dakika ya 22.

Dhidi ya Mbeya City akipasia vyavu dakika ya saba mechi iliyoisha kwa sare ya 2-2.

Mchezo dhidi ya Yanga mchezo wa mzunguko wa kwanza ulioisha kwa sare ya mabao 2-2, alitupia bao dakika ya 42, wakati mchezo dhidi ya Singida United ambao Simba ilishinda 8-0, Kagere alifunga dakika za 1, 25 na 41.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles