30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KAGERE, CHAMA KARANTINI SIKU 14

Asha Kigundula -Dar es salaam

LICHA viongozi wa klabu zenye wachezaji wa kimataifa kutaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupunguza masharti ya wachezaji wa kigeni waliotimkia makwao  kwa ajili  ya mapumziko, Rais wa TFF, Wallece Karia, amesisitiza mchezaji aliyesafiri nje ya Tanzania atakaa karantini siku 14 atakaporejea nchini.

Ili kukabiliana na tishio la virusi vya ebola, TFF imeagiza mchezaji yoyote wa kigeni anayecheza soka hapa nchini aliyesafiri nje ya Tanzania, kufikia sehemu maalum ya uangalizi kwa muda wa wiki mbili atakaporejea nchini.

Hatua hiyo ni wazi itawakuta baadhi ya wachezaji wa klabu za Simba, Yanga na Azam, ambao walitimkia makwao  baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimama.

Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zimesimama, baada ya Serikali kupiga marufuku kwa siku 30 shughuli zenye mikusanyiko ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona, ambao umeuwa maelfu ya watu duniani, tangu uliporipuka kwa mara ya kwanza nchini China.

Hatua hiyo imezilazimisha klabu za soka nchini kuwapa mapumziko wachezaji wao kwa kipindi cha siku 30.

Jana Rais John Magufuli akihutubia Taifa, alisema idadi ya watu waliobainika kuambukizwa  corona hapa nchini imefikia 12.

Akizungumzia na MTANZANIA  jana, Karia alise alisisitiza  wachezaji wa kgeni waliosafiri katika mataifa yao kufikia sehemu maalum  ambako watafanyiwa uchunguzi wa afya ili kubaini kama wana maambukizi ya corona kabla ya kuungana na wenzao.

Alisema ameshangaa kusikia kuna baadhi ya makocha na wachezaji wamesafiri katika nchi zao, wakati  hakuna aliyepewa ruhusa ya kutoka nje ya Tanzania.

Karia alisema hata Rais Magufuli akizungumza na Watanzania alisisitiza hakuna ruhusa ya mtu kusafiri nje ya Tanzania.

Alisema kuna baadhi ya mashabiki wanajisahau kuwa, endapo wachezaji hao wakirudi na maambukizi itakayoendelea kuathirika ni Tanzania, ikiwa pamoja na ligi kwa ujumla, hivyo kuchukua hatua kwa upande wao ni sehemu ya kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.

“Hakuna ambaye amepewa ruhusa ya kutoka nje ya nchi kwani sio likizo bali ni sitisho la muda kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi ya corona, hivyo kwa kocha au mchezaji ambaye ameatoka nje ya nchi hataruhusiwa kujiunga na wenzake mpaka akae sehemu maalum kwa wiki mbili na atajilipia kila kitu,” alisema Karia.

Yanga kupitia kwa Mhamasishaji wao, Antonio Nugaz, alisema wao ni miongoni wa timu yenye wachezaji waliosafiri nje ya Tanzania ambao waliondoka baada ya kutangazwa kusimama kwa ligi kwa kipindi cha siku 30.

Wachezaji wa Yanga waliotimkia katika mataifa yao ni Haruna Niyonzima(Rwanda) na David Molinga wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) pamoja na kocha wao Luc Eymael, wakati kwa Simba ni Meddie Kagere(Rwanda), Clatous Chama(Zambia), Sharaf Shiboub(Sudan) na Luis  Miquissone, Msumbiji.

Wachezaji saba wa Azam nao wametimkia makwao akiwemi  Razak Abalora(Ghana), Nicolas Wadada(Uganda),  Bruce Kagwa(Zimbabwe), Mohamed Yakubu(Ghana), Danny Amola, Donald Ngoma(Zimbabwe) na Never Tigere, Ivory Coast.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mromania Aristica Cioaba na msaidizi wake Vivian Bahati, pia wamesafiri nje ya Tanzania..

Ofisa Habari wa Azam,  Zakaria Thabit Zaka Zakazi, alisema  kwa upande wao waliwapa ruhusa wachezaji wao wote baada ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,  TFF  na Bodi ya Ligi kutangaza, kusimama kwa mashindano kwa siku 30.

“Tuliwapa nafasi maana hata mechi za kirafiki hakuna, ndiyo maana tuliwaruhusu tutafanya mawasiliano  hivyo watarudi kwa muda ili waweze kukaa karantini kama utaratibu uliyopangwa,”alisema Zaka za Kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles