31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KAGERA YAANZA KUTENGA MAENEO YA UFUGAJI

Na RENATHA KIPAKA

SERIKALI mkoani Kagera imeanza kubainisha maeneo ya malisho ya mifugo Wilaya ya Muleba   kudhibiti tatizo la uvamizi holela wa misitu ambayo imetengwa kwa ajili ya hifadhi ya taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu, alisema kwa sasa yameanza kubainika maeneo ya malisho na   yataendelezwa kwa lengo la kuufanya ukanda wa eneo la Mwisa kuwa la wafugaji wenye tija na endelevu wenye tija.

Alisema pamoja na kuwatengea wafugaji maeneo pia watahakikisha wanaviendeleza vijiji vinavyozunguka eneo hilo   kwa kupunguza umasikini kwa wananchi wake.

Jenerali Kijuu alisisitiza kuwa wafugaji watakaopewa maeneo hayo watapaswa kufuga kisasa.

“Tunabainisha maeneo haya ili kuyatenga kwa lengo la kuondoa ufugaji holela na ukataji miti ovyo.

“Tutawawezesha wafugaji wafuge kisasa na kuuendesha ufugaji kama biashara bila ya kuharibu mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho,” alisema.

Aliyataja maeneo mengine kuwa ni katika Ranchi ya Kagoma kwenye bonde la Ziwa Burigi hadi katika Pori la Akiba la Burigi lenye zaidi ya ukubwa wa hekta 60,000.

RC alisema  kuwa ili kuondoa migogoro katika maeneo hayo serikali itayatenga katika vitalu kwa kuweka alama kulingana na jiografia ya eneo husika kuwawezesha kupatikana malisho na makazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles