31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KABURU MUNGU ANAKUONA UJUE

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


KILA shabiki na mwanachama wa klabu ya Simba anayaelekeza masikitiko yake kwa viongozi wa klabu hiyo kutokana na  kuukosa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, wakiamini watani zao wa jadi Yanga hawakuwa na sifa ya kutwaa ubingwa huo.

Simba hadi sasa wamefikisha misimu mitano bila ubingwa wa Ligi Kuu tangu walipochukua mara ya mwisho msimu wa 2011/12.

Wakati huo watani zao wa jadi wamechukua mara nne, moja likienda kwa Azam FC kwa mara ya kwanza msimu wa 2013/14.

Kipindi chote hicho mashabiki na wanachama wa Simba lawama zote wamekuwa wakiwatupia viongozi wao kwa kile walichokiita uzembe kwa kushindwa kunyanyua ubingwa huo na kuwaacha watani zao wakitamba mtaani.

Tofauti na miaka mingine, msimu huu viongozi wa Simba wameonekana kuukomalia ubingwa huo kweli kweli jambo ambalo lilianza kuwaogopesha hata wapinzania wao Yanga.

Viongozi hao walikuwa wakiuukomalia ubingwa huo kwa sababu tatu kwanza kisiasa ili kupata turufu ya kurejea  tena  madarakani pili kufuta aiba kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga tatu hamu ya kurejea kwenye michuano ya kimataifa.

Lakini kitu cha kushangaza waalianza kuwaaminisha wanachama na mashabiki wao lazima wachukue ubingwa huo hata kabla ligi hiyo haijafika kwenye michezo ya muhimu ambayo ingeweza kutoa mwanga wa ligi hiyo inavyoelekea.

Hata baada ya kupoteza baadhi ya michezo hiyo muhimu viongozi hao bado waliendelea kuchangishana fedha wakiwaaminisha mashabiki wao kuwa  ni aina ya ushawishi kwa wachezaji, ilhali baadhi ya viongozi walidaiwa kutumia fedha hizo za michango kwa matumizi binafsi.

Lawama nyingi zinaelekezwa kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kwani ndio mwenye majukumu ya kusimamia masuala yote ya fedha na  mikataba ya klabu hiyo.

Kaburu pamoja na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, wamekuwa wakicheza na hisia za mashabiki wa Simba hasa kwa sababu ya kuifaham kiu yao ya kutaka kunyakuwa taji hilo msimu huu.

Kuzima hasira za mashabiki wao wakaona suluhisho kuegemea kivuli cha kubadili hoja na kujifanya wanapeleka malalamiko yao Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA).

kupeleka malalamiko yao kwenye mahakama ya  soka ya Shirikisho la soka la Kimataifa (CAS) waliamini huenda huko watapata haki walizozikosa katika  Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Malalamiko yao ni pamoja na  maamuzi ya Kamati ya Nidhamu na Adhi za wachezaji ya TFF kupindua uamuzi ulifanywa na Kamati ya Saa 72 ya shirikisho hilo kuhusu pointi tatu za Kagera Sugar.

Kitendo hicho kilishika kasi sana hasa baada ya watani zao kutwaa taji ya ubingwa  msimu huu, kwa viongozi hao kudai  hawautambui ubingwa huo hadi hapo FIFA watapokafanya uamuzi kuhusu malalamiko waliyoyawasilisha.

Lakini baada ya FIFA kutoa pongezi za ubingwa kwa Yanga, mambo yameanza kubadilika kwa viongozi hao kudai  kwamba hawana mpango na ubingwa msimu huu.

Wasivyokuwa na aibu, wanathubutu kusema hawakwenda FIFA kupata ubingwa bali  kuona matumizi sahihi ya kanuni kutoka katika vyombo vya mpira vinasimamia maamuzi sahihi kwa ueledi katika soka.Kwanini hawakufafanua mapema?

Wamesusia zawadi za medali za mshindi wa pili na wachezaji wao kushindwa kuzawadia kihistoria uwanjani, pia kupokea zawadi walizotakiwa kupata baadhi ya wachezaji walioshinda tuzo za msimu.

Upuuzi wao ni dalili za kushindwa kuwa na uvumilivu wa masuala ya soka ndani na nje ya uwanja na matokeo yake wakaanza kusuasua kama watoto yatima.Mungu anawaona mjue.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles