24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

K-Finance yawafunda wanawake wajasiriamali

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ZAIDI ya wanawake 100 wamefaidika na mafunzo ya ujasiriamali yaliyolenga kumfanya mjasiriamali kutumia mtaji wake vizuri na kuiongezea thamani biashara yake.

Mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, yalitolewa na Kampuni ya K-Finance inayojishughulisha na mikopo na mafunzo kwa wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi wa K-Finance, Devotha Minzi alisema mafunzo hayo pia yana lengo la kumfundisha mjasiriamali kuelekea kwenye uhuru wa fikra ya kiuchumi.

Alisema mafunzo hayo pia malengo yake ni kumfanya mjasiriamali aweze kutumia mtaji wake vizuri kwa sababu kumekuwa na matumizi mabaya ya neno ujasiriamali kuwa mjasiraiamali ni kama mtu mwenye biashara ndogo ndogo lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali si biashara ndogo ni namna ya ufanyaji biashara wenye tija.

“Haya mafunzo yetu tumeyaita ‘Ignite Business Clinic’ kwa misingi kwamba ni Kliniki ya kiuchumi, kliniki ya utajirisho, hapa tunatengeneza jukwaa la majadiliano, kuna mambo mengi ambayo Watanzania tunayachukua kama kwa juu juu tu.

“Kwa mfano hatuheshimu watu waliofanikiwa katika jasho na damu watu wanafanya kazi ndiyo wanafanikiwa lakini utasikia mtu anazungumzia mambo kirahisi rahisi tu, unapiga dili kupata fedha, sisi hiyo tunataka tuikemee fedha zinapatikana katika kazi, katika kuongeza thamani ya bidhaa yako.

“Tuliona wakati wanafundisha tusifundishe nadharia tu, sasa huu ni mwaka wa 12 na tunatimiza muhula wetu wa pili kwa hiyo katika mafunzo haya ambayyo tumeanza kwa kina mama lakini tutaenda kwa kina baba na vijana pia, tunataka kubadilisha fikra za Watanzania.

“Tumeanza na wamama kwa kuwa tunatambua mchango wa wanawake katika jamii, mwanamke akishajua kwamba hapa ni kazi na kazi kimpango kazi anaifanya kwa usahihi na pia kwa sababu wao ni walimu,” alisema Devotha.

Kwa upande wake Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Herieth Kitana alisema kumekuwa na dhana potofu kuhusu uwekezaji nchini kuwa mwekezaji ni mgeni kutoka nje, lakini mwekezaji ni mwekezaji tu kinachotofautiana ni mitaji kwamba unawekeza mtaji gani.

taifa limegundua umuhimu wa mwanamke hivyo halijamuacha nyuma katika kukuza uchumi wa Tanzania ndiyo maana hakuna sekta ambayo haina mwanamke.

“TIC inahamasisha sana uwekezaji na kwa mwaka huu tunahamasisha sana sera ya uwekezaji wa viwanda katika madawa lakini pia pia hatutaki mwanamke abaki nyuma kwenye huo uwekezaji asije akafikir
kituo hicho kinafanya kazi ya kushawishi na kuishaurui serikali kuhusu uwekezaji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles