23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

JUMUIYA YA WAFANYABISHARA KUFANYA UTAFITI

PATRICIA KIMELEMETA Na CHRISTINA GAULUHANGA

DAR ES SALAAM

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) inatarajia kufanya utafiti   idadi ya wafanyabiashara waliofunga maduka yao kutokana na kushindwa kuendesha biashara kutokana na ukosefu wa fedha.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya baadhi ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kwa madai kuwa mzunguko wa fedha za ndani ni mdogo, jambo ambalo limechangia kupata hasara.

Akizungumza na   MTANZANIA    katika mahojiano maalumu   Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT), Johnson Minja alisema   kutokana na hali hiyo, idadi kubwa ya wafanyabiashara wameamua kuacha biashara zao na kuendelea na shughuli nyingine kutokana na hali ngumu ya maisha.

“Mzunguko mdogo wa fedha za ndani umechangia baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kuendelea na shughuli zao na kuamua kufunga maduka jambo ambalo linatufanya tufanye utafiti  tuweze kupata takwimu halisi,”alisema Minja.

Alisema tatizo hilo limejitokeza katika kipindi hiki ambacho serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwamo ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) na ununuzi wa ndege.

Alisema miradi hiyo si mibaya  ila tatizo lililopo ni kwamba, uwekezaji wake umefanya mzunguko wa fedha za nje kuwa mkubwa kuliko wa ndani hali inayosababisha upatikanaji wa fedha za ndani kuwa mdogo ikilinganishwa na kipindi kilichopita.

“Kuna wafanyabiashara wamechukua mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha lakini wameshindwa kurudisha kutokana na ukata unaowakabili, jambo ambalo limewafanya wafunge maduka.

“Miradi hii ni mikubwa ambayo inachangia kukua kwa uchumi, lakini serikali ilipaswa kuhakikisha   mzunguko wa ndani unabaki kama ulivyokua awali jambo ambalo lingesaidia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles