23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM KUZINDUA MRADI WA MAJI MUSOMA

Na SHOMARI BINDA – MUSOMA

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwele, ametembelea mradi wa maji wa Bukanga katika Manispaa ya Musoma Vijijini, ambao umekamilika na kuahidi kuwa utazinduliwa na Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua mradi huo, Kamwele alisema ameridhika na ukamilishaji wake kwa asilimia 95 na kubainisha kuwa utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji 36,000 kwa siku.

Alisema mradi huo ambao umegharimu Sh bilioni 45, umekamilika kwa wakati na kubainisha kuwa utawasaidia wananchi wa Manispaa ya Musoma na vijiji 21 vya Wilaya ya Butiama kuondokana na adha ya maji.

“Nimpongeze sana kandarasi na wasimamizi wa mradi huu ambao ni mkubwa, hakika wamefanya kazi nzuri kuondoa kero ya maji kwa wananchi, huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma ya maji katika maeneo yao.

“Hivyo tatizo la maji kwa mji wa Musoma na maeneo mengine tayari limepata ufumbuzi, sasa tunaendelea kujipanga kwa maeneo mengine ili kuhakikisha Watanzania wanapata maji safi na salama, lakini jambo la muhimu ni wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji,” alisema.

Aidha Kamwele alisema kwa sasa Serikali imesimama kikamilifu kuhakikisha taasisi za umma zilizokuwa hazilipi madeni yake ya ankara za maji kiasi cha kudaiwa zaidi ya Sh bilioni 40, zinaendelea kulipa na kumaliza madeni yao.

Awali akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa), Said Gantala, alisema licha ya changamoto zilizokuwapo katika mradi huo, bado wameweza kuukamilisha kwa wakati ili uanze kutoa huduma kwa wananchi.

Alisema baada ya kukamilisha hilo, sasa watahakikisha wananchi wanaunganishwa na huduma ya maji na kuwaomba kutoa ushirikiano kufanikisha  kutandazwa mabomba ya maji kwenda kwenye makazi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles