JPM AWAKUMBUKA WASIRA, LIMBU

0
931

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


RAIS Dk. John Magufuli amemteua waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya nne, Stephen Wasira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana, ilieleza kuwa Wasira anachukua nafasi ya Profesa Mark Mwandosya.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dk. Festus Bulugu Limbu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (National Economic Empowerment Council – NEEC).

Dk. Limbu anachukua nafasi ya Dk. John Jingu ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto).

Taarifa ilieleza zaidi kuwa uteuzi wa viongozi hao umeenza jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here