25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AUNDA ‘JESHI’ JIPYA CCM

Na MWANDISHI WETU – Dar es Salaam             |         


 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, ni kama ameunda ‘jeshi’ jipya la siasa ndani ya chama hicho, ambalo linatazamwa kumsaidia katika masuala ya kisiasa na hata kumvusha wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Tafsiri ya kuundwa kwa ‘jeshi’ au kwa lugha nyepesi timu ambayo inatajwa kuwa kitovu cha kumsaidia ndani ya chama hicho, inabebwa na mtazamo wa kuwapo sura nyingi mpya katika uteuzi uliofanywa wiki hii katika Sekretarieti ya CCM Taifa, na Kamati Kuu (CC).

Kinachoakisi hilo pia ni uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Dk. Bashiru Ally, ambaye naye aliteuliwa wiki hii kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

Dk. Bashiru ambaye ni mwanazuoni mbobezi katika masomo ya sayansi ya siasa, amechukua nafasi hiyo baada ya Kinana kumwandikia barua Mwenyekiti wake, Rais Magufuli ya kumwomba apumzike.

Ujio wa Dk. Bashiru unamuunganisha na sura mpya nyingine zilizomtangulia ndani ya Sekretarieti hiyo ya CCM, akiwamo Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Ngemela Lubinga.

Wengine anaoungana nao ni Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Dk. Abdallah Juma Mabodi, Naibu Katibu Mkuu (Bara), Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha, Dk. Frank Haule na Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni, Pereira Ame Silima.

Ukiachia mbali Sekretarieti, pia mtazamo huo wa kujenga ‘jeshi’ la ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles