27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM atinga kwa Mzee wa upako

JPM atinga kwa Mzee wa upakoNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli ametembelea Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji, Antony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ lililopo Ubungo Kibangu   Dar es Salaam na kuahidi kutengeneza barabara inayopita karibu na kanisa hilo.

Alitoa ahadi hiyo kwa waumini wa kanisa hilo jana akisema Serikali yake itatengeneza barabara ya kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side ambako inaungana na barabara ya Mandela.

Akizungumza  katika ibada hiyo, Rais alisema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine   kujionea hali halisi.

Rais Magufuli pia alitumia fursa  hiyo kumpongeza kiongozi huyo wa kiroho kwa huduma ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia vipindi vyake vya mahubiri kupitia runinga.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.

“Ndiyo maana kuna siku moja ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi.

“Nikamtuma meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu…nataka kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo, alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na waumini.

Naye Mchungaji Lusekelo alimshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa hilo na kumuombea heri katika uongozi wake   aweze kufanikisha azma ya kuliletea taifa maendeleo ukiwamo mpango wa kuanzisha viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles