27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

JPM aonya majaji kesi za ‘mshiko’

Na NORA DAMIAN

-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amewatahadharisha majaji na mahakimu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kutaka kupangiwa kesi zenye mwelekeo wa rushwa.

Alisema bado makosa ya uaminifu, uadilifu na kukosa kuwajibika kwa baadhi ya watumishi wenye mamlaka ya kutoa haki na dhamana yamendelea kutokea.

Akizungumza jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria, alisema baadhi ya wasajili wa mahakama wamekuwa wakichagua mahakimu na majaji wa kuwapelekea kesi zenye mwelekeo wa utoaji rushwa.

“Wasajili wa mahakama na ninyi kuna dhambi zenu ndogondogo ambazo zipo kazirekebisheni.

“Na saa nyingine mnachagua jaji gani apelekewe kesi, huyu anapelekewa kesi yenye mshiko na mwingine ya shuruba, mkatende haki,” alisema Rais Magufuli.

Alisema wanasheria pia wana mtindo wa kushirikiana na kumpora haki asiye na hatia.

“Lakini pia wanasheria siku zote huwa kuna pande mbili. Mwanasheria wa utetezi na upande mwingine.  Wanafanya ‘discussion’ (majadiliano) usiku, wanazungumza kuhusu kesi itakavyokwenda ili kusudi amuache mwanasheria wa kujitegemea ashinde kumbe kuna mgawo.

“Dhamira zenu ziwasute, hamzikosei roho zenu tu, mnamkosea Mungu, tukazingatie maadili ya kazi zetu,” alisema.

Pia alikemea tabia ya ucheleweshaji kesi ambayo imesababisha kesi 1,989 kufutwa mwaka jana kwa sababu ya kukaa muda mrefu mahakamani.

“Kapelelezeni haraka, umekiona kitu kipo unakwenda kupeleleza nini, mtu ameshikwa anaiba na kidhibiti anacho bado unataka ukapeleleze alivyoiba alikuwa ameinama au amelala.

“Mtu anashikwa na meno ya tembo, dawa za kulevya wanasema mpaka tupeleke kwa mkemia mkuu na vinapozidi kukaa kwa mkemia mkuu wanasema ni majivu si dawa za kulevya,” alisema.

Alisema wakati mwingine waendesha mashtaka wamekuwa wakitumia mbinu ya kusema upelelezi bado unaendelea kwa lengo la kumshawishi mshtakiwa kutoa rushwa.

“Lawama wanapewa mahakimu na majaji wana…

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles