28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AMPA DK. SLAA UBALOZI

Na ELIZABETH HOMBO


WIKI chache baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, kuajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, hatimaye Rais Dk. John Magufuli amemteua kuwa balozi.

Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2105.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana jioni, Dk. Slaa ataapishwa baada ya taratibu kukamilika.

“Rais Magufuli amemteua Dk. Slaa kuwa balozi, ataapishwa baada ya taratibu kukamilika,” ilisema taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya Ikulu haikusema Dk. Slaa atakuwa balozi wa nchi gani.

Alipoulizwa na gazeti hili kwa simu kuhusu uteuzi huo jana, alijibu kwa kifupi: “Mungu wangu.”

Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu uteuzi huo, alisema hana maoni kwa sasa.

Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu na mgombea urais wa Chadema mwaka 2010, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket.

Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya Sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu katika mahojiano maalumu, Dk. Slaa, alisema kuwa kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.

Hata hivyo, Dk. Slaa, ambaye alipata kuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

Septemba 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa, alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya Chadema juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles