25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

JPM aahirisha sherehe za Uhuru mwaka huu, fedha za maandalizi kujenga hospitali Dodoma

Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli, ameahirisha maadhimisho ya siku ya Uhuru kwa mwaka huu na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shamrashamra hizo ameelekeza zitumike kujenga hospitali mkoani Dodoma ambayo itaitwa Hospitali ya Uhuru.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Novemba 20, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Magufuli ameagiza kiasi cha Sh milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo Desemba 9 mwaka huu, zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa mkoa wa Lindi pamoja na wilaya zake katika kikao cha maandalizi ya shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru mkoani Lindi.

“Hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo na Chamwino kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam itakuwa inawahudumia wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wananchi wengine watakaokuwa mkoani humo,” amesema Waziri Mkuu katika taarifa hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mkuu amesema Rais Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuandaa matukio watakayoyatekeleza katika maeneo yao yatakayoashiria maadhimisho ya siku ya Uhuru.

“Wanaweza kutumia siku hiyo kwa kufanya usafi maeneo ya wazi au kwenye hospitali.

“Wananchi pia katika maeneo yote nchini wajiandae kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zitakazopangwa na wakuu wao wa mikoa na wilaya kufanyika katika maeneo yao,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles