31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Joto la urais lapanda Z’bar

HamadRashidMohammedNa Mwandfishi Wetu, Zanzibarr

JOTO la kuwania urais wa Zanzibar limezidi kupanda huku mgombe wa nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamesd  akijitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Hamad ametamba kuwa anatarajia kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuanzisha shirika jipya la ndege la Zanzibar iwapo wananchi watampigia kura kuwa Rais mpya katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Hamad alitoa msimamo huo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania urais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchguzi Zanzibar(ZEC),  Salim Jecha Salim katika ukumbi wa Bwawani mjini Zanzibar.

Alisema sera ya msingi ya ADC katika masuala ya kiuchumi ni kuhakikisha Zanzibar inakua na kusongambele kiuchumi kwa kutumia rasimali ardhi, utaalamu na maliasili zake ikiwemo usimamiaji bora na program endelevu katika maeneo ya sekta za kilimo, bahari, usafiri wa anga na utalii.

“Sera yetu ADC hatusubiri utekelezaji wa masuala ya msingi yanayogusa maisha ya watu katika kujenga uchumi kwa kusubiri hadi tuingie ikulu, mimi na SMZ yatari tumeshapeleka wataalam wawili China kuansiaha mchakato wa kuianzisha shsirika la ndege la Zanzibar,” alisema Hamad.

Alisema iwapo atapata ridhaa ya kuwa rais atakuza kilimo cha karafuu, manukato , kuboresha sekta za uvuvi, ujenzi wa viwanda vya kuhifadhi na kusindika samaki ikiwemo pia kutanua wigo wa utalii.

“Nikishinda urais nitahakikisha nadumisha na kuendeleza misingi ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa manufaa ya wazanzibar wa kizazi cha cha sasa na kijacho,”alisema

Mgombea mwingine wa urais Mohamed Masoud Rashid wa Chama cha CHAUMA alisema akibahatika kuwa rais mpya atabadilisha mfumo mzima wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar na kuufanya kuwa na uwakilishi wa umoja wa kitaifa badala ya kuvishirikisha vyama viwili vya CCM na CUF peke yake.

 

Masoud pia alisema ipo haja na ulazima wa kubadili sera na mipango ya kujenga uchumi kuwa ya kitaifa badala ya kuhodhiwa na chama cha siasa kinachotoa rais.

“Haiwezekani kwa muundo wa muungano wa kondoo 99 kwa mmoja, tunataka muungano wa serikali tatu huku kila upande ukiamua mambo yake bila kuingiliwa na upande mwingine,” alisema Masoud

Kwa pande wake Mkurugenzi wa ZEC Salum Kassim alisema hadi sasa ZEC imepokea majina ya wagombea 12 wanaotaka kuwania urais wa Zanzibar ambapo hadi jana jumla ya wagombea watano walikabidhiwa fomu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles