25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate ala shavu tuzo za SZIFF

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amechaguliwa kuwa mlezi wa tamasha la tuzo la Kimataifa la Sinema Zetu (SZIFF), ambapo mchakato wake utaanza Januari 1 hadi 15 mwakani na kuhitimishwa kwa usiku wa tuzo utakaofanyika Februari 23 mwakani.

Katika tuzo hizo washiriki kutoka nchi sita za afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Congo, Rwanda na Burundi ambapo vipengele 24 vitashindaniwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo, leo Septemba 25, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema wamemchagua  Mwegelo kuwa mlezi wao kwa sababu aliwahi kushiriki katika kazi za sanaa hizo na ana uelewa mkubwa katika tasnia ya filamu.

“Tamasha hili ni la kwanza kwa filamu Afrika kuoneshwa kwenye televisheni, filamu zitashindanishwa katika vipengele tofauti huku ushindani ukiaminika kuwa mkubwa zaidi ya msimu uliopita. Moja ya kigezo cha filamu zitakazoshindanishwa ni lazima ziwe zimeandalia kati ya mwaka 2016 na 2018 maana kwa hali hiyo itatupa picha halisi ya ufanisi na ubora wa waandaaji wa filamu,” amesema mhando.

Naye Mwegelo akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa mlezi wa tamasha hilo, amesema yeye kama mlezi kazi yake kubwa ni kuhamasisha vijana wafanye kazi nzuri ili kukuza tasnia ya filamu na wajipatie kipato kikubwa pia.

“Naushukuru uongozi mzima wa Azam kwa kunichagua kuwa mlezi wa tamasha hili, kwa kweli nimepata faraja na kazi yangu kubwa tofauti na ulezi ni kuhamasisha vijana wafanye kazi nzuri za sanaa zitazoweza kuinua tasnia ya filamu na kuitangaza nje ya mipaka ya nchi yetu,” amesema.

Aidha Mratibu wa tamasha hilo, Sophia Mgaza ameelezea kuwa dhumuni kuu la kuleta soko la filamu na televisheni chini ya mwamvuli mmoja ambapo inaenda sambamba na kampeni iliyopewa jina la ‘Lugha moja, Taifa moja’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles