JKT YAIFUNGIA KAZI NBL

0
33

Na SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM

KOCHA wa timu ya kikapu ya JKT, Alfred Ngalaliji, yuko katika maandalizi kabambe kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Taifa ya mchezo huo inayotarajia kaunza Novemba 16  kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ngalaliji alisema wana wiki ya pili sasa tangu wameanza mazoezi hayo ndani ya uwanja wa klabu ya Jeshi ABC maarufu  95.

“Novemba 16 hadi 22 itaanza ligi ya NBL inayosubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wa kikapu ndani na nje ya Tanzania, ni ligi kubwa kwa hapa nyumbani hivyo tunaendelea na mazoezi kujihakikishia ubingwa,” alisema Ngalaliji.

Ngalaliji anatoa wito kwa timu pinzani, kutotegemea mteremko kutoka kwao badala yake wajiandae kupokea kichapo katika kila mchezo pindi watakapokutana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here