31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JKT Tanzania washtuliwa

Theresia Gasper -Dar es salaam

TIMU ya JKT Tanzania imechapwa mabao 2-0 na Zimamoto, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi.

JKT ipo Zanzibar ikijifua kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohammed ‘Bares’, alisema anahitaji mechi zaidi za kirafiki ili kikosi chake kiweze kuimarika.

“Tumecheza mchezo mmoja dhidi ya Zimamoto lakini tumefungwa 2-0, ila ndio kwanza tumeanza kucheza mechi za kirafiki.

“Naamini tutafanya vizuri katika michezo ijayo,” alisema.

Alisema amesajili kikosi kipana ambacho anaamini kitaleta ushindani katika Ligi Kuu msimu ujao tofauti na walivyokuwa msimu uliopita.

Bares alisema kwa kipindi hiki kifupi walichoweka kambi Zanzibar,  ameanza kushuhudia  mabadilika ya kiuchezaji katika kikosi chake.

JKT msimu uliopita ilimaliza Ligi Kuu ikiwa nafasi ya kumi, baada yta kujikusanyia pointi 47.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles