26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

JKCI, Marekani yafanya upasuaji kwa wagonjwa 25

AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete  (JKCI), wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani kwa mara ya kwanza wanatarajia kufanya upasuaji Mkubwa wa moyo  kwa watu 25 hadi 30 katika kambi ya siku 13.

Akizungumza na MTANZANIA jana Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk. Angela Muhozya alisema tangu kuanza kambi hiyo Januari 13 tayari watu 15 wameshafanyiwa upasuaji.

“Hii timu ya upasuaji watoto na watu wakubwa inafanyika hapa  ili kuweza kubadilishana uzoefu wa kufanya opareation kubwa ambazo hatujawahi kuzifanya .

“Tunatarajia kufanya upasuaji kwa watu 25 hadi 30 na tunafanya oparation kubwa ambazo zingine hatujafanya na zingine ambazo tumefanya lakini nihatarishi sana kwa wiki hii tutafanya nyingine Profesa na baadae watafanya madaktari wazawa atawasimamini mpaka sasa tumefanya oparation 15 watoto nane na watu wazima saba kwa wiki iliyopita,” alisema Dk. Muhozya.

Alisema kuwa upasuaji mkubwa inayofanyika ni wa  kupandikiza mishipa kwa watoto, kuziba matundu na upasuaji mkubwa wa fontan ambao  unafanyika kwa hatua ya kwanza na ya pili ya kuunganishwa mishipa.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto  (JKCI), Godwin  Sharao, alisema kuwa upasuaji huo mkubwa umekuwa ukurahisisha matibabu ya moyo kwa watoto.

“Upasuaji wa aina ya fontan huwa ina hatua ya pili ya kukamilisha kutengeneza mfumo mpya wa mzunguko wa damu ambapo damu inaporudi kutoka mwilini inaenda moja kwa moja kwenye mapafu na haiendi upande wa kulia wa moyo.

“Sasa watoto hawa tunawafanyia hivyo kutokana na upande wa kulia wa moyo kuwa na tatizo kwahiyo tunatumia njia hiyo ili damu isiende upande wa kulia isichafuke ,tunataka damu hiyo ipate oksijeni kwenye mapafu kuna mishipa miwili mikubwa ambayo mmoja unaitwa ‘ superial venacav’inarudisha damu kutoka kwenye kichwa na mikono kurudi kwenye moyo na mwingine unatoka miguuni na tumboni tunaota ‘infernal venacav’.

“Kufanya upasuaji hii inastage mbili kwanza unganisha mishipa mkubwa wa juu hadi kwenye mapafu halafu tunamwacha mtoto aende lakini akifikishwa miaka mitano anatakiwa arudishwe kufanya upasuaji wa kuunganishwa unaotoa damu sehemu za chini na kuunganishwa na mapafu,” alisema

Alisema mfumo upasuaji wa aina hiyo kunamfanya mtoto asipate kukonda mara ya pili kutokana na kutumiamia tundu dogo kwa upasuaji wa pili.

“Katika mfumo huu mpya tunatengeneza mshipa wa bandi tunaunganisha na tunatengeneza kikuta dhaifu  ambayo hairuhusu damu kwenda kwenye mapafu inakuwa kama tumefanya njia moja kwa mzunguko wa damu.

“Baada ya mwezi mmoja mtoto atarudi hospitali  na tutatumia tundu dogo kupitisha mirija ambayo utaenda kutoboa ule ukuta dhaifu baada ya hapo hali yake inakwenda vizuri,” alibainisha Dk. Sharia.

Alisema kutokana na kambi hiyo wanaendelea kupata mafunzo kwa madaktari wasiku nyingi na wenye uzoefu mkubwa hiyo watasaidia katika utoaji wa huduma mpya.

“Wiki hii tutafanya sisi wazawa na yeye atakuwa anatusimamia hii teknolojia inapunguza maumivu ya vidonda ,kukaa hospitali muda mrefu, itaokoa hela za kukaa mda mrefu hata hivyo Stage ya kutoboa ukuta bado ni geni tunataka tuwafanyie watoto wengi ili madaktari wetu wanaposhirikiana na wengine waweze kupata hiyi procedure vizuri,” alisema

Naye Daktari Bingwa wa upasuaji watoto kutoka Marekani ambaye pia ni mgunduzi wa aina hiyo ya upasuaji mkubwa Profesa Donato Sisto, aliwahimiza madaktari kupenda kazi yao ili waweze kuhudumia wagonjwa vizuri.

“Kuwa daktari ni kuwapenda watu huwezi kuwa daktari ila kupenda ndugu zako ili uweze kuwasaidi kufanya maisha yao kuwa ya furaha kwangu mimi ninafanya kila liwezekanalo kuhakikisha watu wanapoona na hii kazi naifanya kwa moyo wangu wote ndio maana niko leo kuwasaidia wengine,” alisema Prof. Sisto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles