31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jipu latumbuliwa Baraza la Michezo

napeNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henry Lihaya, baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya jana katika ofisi za BMT kuona miundombinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.

“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,” alisema Waziri Nnauye.

Alisema miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.

Kutokana na utenguzi huo, Waziri Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT, Dionis Malinzi, kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.

Vile vile Waziri Nnauye amemtaka Mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.

Aidha, amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles