30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI YA KUSHAWISHI MTOTO KURUDI SHULE BAADA YA LIKIZO


NA AZIZA MASOUD

MWEZI mgumu umewadia, kila mzazi mwenye mtoto/ watoto wanaosoma anahangaika kufanya maandalizi ya vifaa vya shule kwaajili ya watoto.

Sambamba na watoto waliokuwa likizo baadhi ya wazazi wanawaandaa watoto wanaoingia darasa la kwanza  au kidato cha kwanza.

Maandalizi ya watoto hasa wanaoanza darasa la kwanza ni tofauti na wale wanaoingia madarasa mengine.

Kwa kawaida baadhi ya watoto wanaoanza  shule ya msingi huwa wasumbua na wengine huwa na shauku ya kwenda shuleni.

Usumbufu huo upo pia kwa watoto wanaoingia darasa jingine kwani kipindi cha likizo ndefu ya mwisho wa mwaka watoto wengi hushiriki zaidi kwenye michezo, hivyo huona adha kuamka asubuhi.

Sambamba na hilo adha wanazozipata watoto shuleni iwe wakati wa kwenda ama kurudi nyumbani humfanya mtoto asitamani kwenda shuleni.

Sababu ni nyingi nyingine ni uvivu tu wa mtoto baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu  watoto hivyo hutafuta visingizio lukuki ili tu asiweze kwenda shuleni.

Kutokana na hali hiyo wazazi wana wajibu wa kuwaandaa watoto kisaikolojia ili wafahamu kuwa mapumziko yalikuwa ni ya muda tu hivyo wakati umeshafika wa kurejea shuleni.

Wazazi hawapaswi kuwapiga wala kuzidisha ukali bali watumie busara na ushawishi ikiwamo kumuahidi mtoto zawadi.

Mzazi amchukue mtoto/watoto wakati wa kumwandalia mahitaji ya shule ikiwamo kumnunulia viatu, kalamu, vifutio, madaftari, mkebe, rula begi na sare za shule ili mtoto atamani kuvaa au kwenda shule na vitu vipya.

Kama mzazi umejiandaa vizuri kwa maandalizi ya mtoto wako jitahidi kununua kila kifaa anachokitaji.

Mtoto anapoviona  vinamsaidia kupata nguvu ya hata kuwaza masuala ya shule na kutojihisi mpweke anapoanza kuhudhuria masomo yake.

Katika kipindi hiki  ambacho anakaribia kufungua shule jitihadi kumuongelesha masuala ya shule kama changamoto anazokutana nazo katika muhula uliopita  ikiwezekana umuulize anadhani ukimfanyia nini ataweza kufanya vizuri katika masomo yake kwa mwaka huu unaoanza.

Jaribu kumkumbushia mambo mbalimbali  aliyokuwa akiyafanya akiwa shuleni na kuyafurahia.

Maandalizi kama haya yakifanyika kwa ufasaha yatamfanya mtoto aanze kwenda shule akiwa na furaha na amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles