29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI YA KUPIKA WALI WA SAUSAGE NA MAJANI YA VITUNGUU

MAHITAJI

Vipande vya sausage
Majani ya vitunguu fungu 1
Kitunguu kikubwa 1
Njegere gram 100
Mchele basmati gram 500
Chumvi
Pilipili manga

 

JINSI YA KUPIKA

Weka mafuta katika kikaango halafu kaanga vitunguu maji

Ongeza majani mabichi ya vitunguu

Baada ya kukaanga kwa dakika mbili vitunguu pamoja na majani vitoe tu harufu na si kuungua au kubadilika rangi, kisha weka mchele na endelea kukaanga

Kaanga mchele kwa dakika tatu hadi nne kisha weka maji ya wastani yazidi mchele wako kiasi na uendelee kukoroga ili maji yachanganyike na mchele

Baada ya hapo funikia na weka moto wa wastani ili wali uive taratibu

Chukua sausage zako na kata kata vipande vidogo

Tupia juu ya wali wako njegere zilizochemshwa pamoja na vipande vya sausage

Kumbuka kuendelea kukoroga ili kila kitu kichanganyike, pia kama mpenzi wa blue band au samli unaweza weka kiasi ili kuongeza ladha na harufu nzuri katika wali

Baada yahpo funika kwa muda na wali wako utakuwa tayari kwa kuliwa. Ni vema kumpatia mlaji kikiwa chamoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles