24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JILL AOMBA TALAKA KUHOFIA MAISHA YAKE

CALIFORNIA, MAREKANI

MKONGWE wa muziki na filamu nchini Marekani, Jill Scott, ameomba kuachana na mume wake, Mike Dobson, baada ya kufunga ndoa miezi 18 iliyopita.

Jill mwenye umri wa miaka 45, ameweka wazi kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kuona maisha yake yapo hatarini tangu kufungwa kwa ndoa hiyo.

“Nimeamua kuomba talaka kwa kuwa maisha yangu yapo hatarini, tangu niingie kwenye ndoa, Dobson amekuwa wa kunitisha mara kwa mara, malezi yake yamekuwa tofauti na awali pamoja na mambo mengine mengi, hivyo nimeona bora nikae pembeni,” alisema Jill.

Hata hivyo, kwa upande wa Dobson, ameonekana kumshangaa mrembo huyo huku akidai kuwa alikuwa anampa kila kitu ambacho alikuwa anakitaka pamoja na kumhakikishia usalama wa maisha yake, ila anaamini labda kuna jambo lingine tofauti na aliyoyataja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles