33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JIJI LA MWANZA KUNUFAIKA NA MRADI UBORESHAJI

Na CLARA MATIMO- MWANZA

JIJI la Mwanza linatarajia kunufaika kutokana na uboreshaji wa miundombinu ambayo italiwezesha kustahimili katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari za majanga kupitia mradi unaotekelezwa na Taasisi ya Utafiti na Sera ya Governance Links Tanzania.

Alizungumza hayo jana, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Donald Kasongi, wakati akitambulisha mradi huo kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, sekta binafsi, taasisi za serikali na wadhibiti wa shughuli za umma.

Alisema mradi huo wa kujenga ubia wa usimamizi bora wa mazingira na kuimarisha ustahimilivu katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza umefadhiliwa na Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini, kupitia mradi wake wa A Piscca Supported Initiative, kwa gharama ya Sh milioni 77 awamu ya kwanza, kuanzia Oktoba 2017 hadi Septemba 2018.

“Mradi huu utabadilisha fikra za jamii kuhusu umuhimu wa mazingira, tunataka mazingira na majanga yaingizwe kwenye mpango mkakati wa maendeleo ya jiji la Mwanza, nia ya ubia ni kujenga uwezo na uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa ustahimilivu.

“Jamii itarajie kujengewa uwezo wa kukabiliana na majanga kwa haraka zaidi, mbinu mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuweza kutatua changamoto za kiuchumi, kijamii na mazingira, pia kuwe na viwanda vinavyozingatia uendelevu wa  mazingira utakaolifanya jiji hili liwe salama na watu watamani kuishi hapa,” alisema Kasongi.

Kasongi alisema mradi huo ni maandalizi ya mpango wa muda mrefu wa kujenga ustahimilivu kwa sababu miji mingi, likiwamo jiji la Mwanza, inakabiliwa na changamoto ya kuingia watu wengi kwa nia ya kutafuta maisha, hivyo kusababisha  kushindwa kutoa huduma salama inapotokea majanga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles