30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jessie J atarajiwa kuitwa mama

LONDON, ENGLAND



HATIMAYE nyota wa muziki nchini Uingereza, Jessica Cornish, maarufu kwa jina la Jessie J, amewashtua mashabiki wake baada ya kutangaza kuwa anatarajiwa kuitwa mama.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 30, miaka minne iliyopita aligundulika kuwa na tatizo la kizazi na kudaiwa hataweza kupata mtoto katika maisha yake, lakini sasa inadaiwa kizazi chake kipo salama na anaweza kupata watoto.

“Kwa kipindi cha miaka minne nilikuwa katika maumivu makali na huzuni wa kila siku huku ikiwa siri katika maisha yangu, kwa kuwa niligundulika na tatizo la kizazi na nikaambiwa siwezi kupata mtoto.

“Furaha niliyonayo kwa sasa haielezeki, ninatarajiwa kuitwa mama, ninawashukuru wote ambao walikuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu, kweli nimeamini kuna maajabu duniani, nawashukuru sana,” alisema msanii huyo.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumaliza kuimba wimbo wake wa ‘Four Letter Word’ kwenye tamasha la Royal Albert Hall, lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini London.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles