30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi Sudan lashtukia kutaka kupinduliwa

KHARTOUM-SUDAN

BARAZA la kijeshi linalotawala nchini Sudan  limesema limetibua mipango ya mapinduzi yaliyolenga kuzuia mpango wa kuunda serikali shirikishi na makundi ya wapinzani.

Msemaji wa Jeshi la nchi hiyo, Jenerali Jamal Omar amesema watu kadhaa miongoni mwao wakiwamo maofisa wa jeshi wa sasa na wa zamani na wale wa usalama wamekamatwa.

Sudan inakabiliwa na mkwamo wa uongozi tangu Rais Omar al-Bashir aondolewe kwa mapinduzi mwezi Aprili mwaka huu.

Wakati huo huo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limesema limesikia kwamba baraza la kijeshi limehusishwa na mauaji ya waandamanaji.

Katika uchambuzi wake BBC kupitia ‘Africa Eye’ video fupi kupitia simu ya mkononi  inaonyesha mauaji ya Juni 3, mwaka huu yalitekelezwa na kikosi chenye nguvu zaidi kinachojulikana kama ‘Rapid Support Forces’(RSF),  kundi la wanamgambo chini ya agizo la baraza la kijeshi linalotawala.

Katika tukio hilo,  waandamanaji walifyatuliwa risasi na hivyo wengi kupoteza maisha.

Wanaume wawili ambao wanahudumu RSF waliliambia BBC kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa agizo la uongozi wa RSF.

Hata hivyo BBC inasema tuhuma hizo hawawezi kuzithibitisha.

Taarifa hizi mpya zimekuja ikiwa ni takribani wiki mbili zipite tangu wapatanishi wa Umoja wa Afrika waseme majenerali wa kijeshi nchini Sudan wamefikia makubaliano na viongozi wa maandamano juu ya kugawana madaraka.

Makubaliano hayo ya kihitosria yalikuja baada ya mazungumzo ya mwisho kuhusiana na nani anapaswa kuongoza chombo kipya cha utawala kati ya raia na jeshi kuvunjika mwezi Mei.

Chini ya makubaliano hayo mapya  jeshi na upinzani watashirikiana  katika kuongoza serikali hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu na kisha kusimamia uchaguzi huru na wa haki.

Umoja wa Afrika (AU) ulisema katika makubaliano hayo pia wameahidi kuunda serikali huru itakayoongozwa kitaalamu pamoja na kuchunguza ghasia za hvi karibuni zilizosababisha mamia kufariki.

 â€œPia wamekubaliana juu ya serikali huru ya kiraia, inayoongozwa na waziri mkuu msomi, ambayo itakuwa na uwezo na kutumikia taifa,” alikaririwa wiki mbili zilizopita mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Mohamed El Hacen Lebatt katika mkutano na waandishi habari mjini Khartoum.

Naibu kiongozi wa baraza la kijeshi, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo naye alisema makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa hayatambagua yeyote.

Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo ni  naibu mkuu wa Baraza la kijeshi la Sudan, na kiongozi wa kikosi chenye nguvu RSF alisema vyama vyote vya kisiasa na makundi yote ya kivuguvugu ya vijana waliochangia kwenye mapinduzi na wanawake makubaliano hayo yanawahusu.

Lebatt hakuzungumzia muundo kamili wa chombo hicho kipya tawala, lakini kiongozi maarufu wa maandamano Ahmed al-Rabie alisema kitajumuisha raia sita, wakiwemo watano kutoka vuruguvugu la maandamano, na wanajeshi watano.

Lebatt zaidi alizungumzia jinsi pande hizo mbili zilivyokubaliana kuahirisha uundwaji wa Bunge jipya la mpito.

Bunge hilo lina wawakilishi 300, theluthi mbili kati yao wakitokea vuguvugu la maandamano.

Taarifa za makubaliano hayo zilipokelewa kwa shangwe mitaani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles