31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi lawasili mkoani Mtwara kusomba korosho

Nora Damian, Mtwara



Agizo la Rais John Magufuli la kununua korosho zote limeanza kutekelezwa ambapo tayari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewasili mkoani Mtwara kwa kazi hiyo.

Mapema leo asubuhi askari wa JWTZ wamewasili wilayani Newala na kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho yaliyopo wilayani humo.

Askari hao ambao waliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo, walitembelea na kukagua maghala matatu yaliyopo wilayani humo ambayo ni Micromix, Agro Focus na ghala la Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala ( Tanecu).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles