23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jela miaka 60 kwa kulawiti, kuvutisha watoto bangi

MALIMA LUBASHA-MUSOMA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara,imemuhukumu Nyamasheki Malima (41)kifungo cha miaka 60 jela,baada ya kumkuta na hatia ya kuwavutisha bangi watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 11 na 13, kisha kuwala witi.

Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki,Hakimu Jacob Ndira,alisema Malima alitenda makosa hayo kati ya Septemba 2017 na Septemba, mwaka jana, baadaye alikamatwa na kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayomkabili ,lakini alikana kufanya kitendo hicho.

Alisema baba wa watoto hao, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kubaini hali hiyo kwa mtoto mmoja  wapo  akiwa katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kumfanyia uchunguzi  na kuwahoji ndipo walimtaja mtuhumiwa alikuwa akiwafanyia kitendo hicho.

Hakimu Ndira, alisema mahakama ilisikiliza maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kuridhika bila ya kuacha shaka yoyote, huku mshtakiwa akijitetea mwenyewe jambo ambalo ndani yake kulikuwa na uovu umefanyika, ikiwamo kuwaingilia kinyume na maumbile (kuwalawiti).

Alisema ushauri wa daktari aliyewafanyia vipimo watoto hao, ulibainika sehemu ya haja kubwa ilikuwa imeingiliwa kila wakati,baada ya kuvutishwa bangi na kulewa kisha kuwalawiti watoto hao ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.

Kutokana na maelezo ya kina ya kitabibu ya daktari,hakimu Ndira ,alisema mahakama imejiridhisha watoto walileweshwa kwa dawa za kulevya aina ya bangi.

Baada ya maelezo hayo, hakimu aliuliza upande wa mashtaka kama wana jambo lolote la kuieleza mahakama,ndipo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Theophil Mazuge aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine kwani ikizingatiwa makosa ya aina hiyo yamekuwa yakijirudia kwenye jamii.

Hakimu Ndira,alimuuliza mshtakiwa kama ana chochote cha kujitetea kwa nini mahakama impunguzie adhabu, yeye alidai hana nguvu za kiume kwani asingeweza kufanya kitendo hicho na kuiomba mahakama imsamehe.

Baada ya utetezi wake ,Hakimu Ndira alimwambia mshtakiwa hana nama ya kupunguziwa adhabu,hivyo atakwenda jela miaka 60 kutokana makosa mawili ya kuvutisha bangi na kulawiti na atatumiki a kifungo kila kosa muda wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles