22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Japan yasaidia biloni 170/- kwa Profesa Muhongo

Profesa Muhongo
Profesa Muhongo

NA SHOMARI BINDA,

SERIKALI ya Japan imetoa Sh  bilioni 170 kwa ajili ya uboreshaji wa  miundombinu  na kuweka vifaa vya huduma bora katika  Kituo cha afya Murangi katika  Jimbo la Musoma vijijini.

Fedha hizo zilitolewa jana na  Balozi wa Japan  nchini, Masaharu Yoshida  ambaye alisema lengo ni kuiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma stahiki kwa  kila mwananchi.

Alisema  fedha hizo zitatumika  kuboresha miundombinu, kujenga nyumba za wauguzi, choo cha wagonjwa, shimo la kutupia kondo la nyuma na kurekebisha tanuru la kuchomea takataka  za hospitali ikiwa lengo ni kuweka mazingira  safi na salama kwenye kituo hicho.

Yoshida alisema suala la afya ni jambo la  msingi kwa maisha ya binadamu.

Alisema  msaada huo unatokana na ombi la  Mbunge wa   Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni  Waziri wa Nishati na Madini.

Yoshida alisema ikiwa kituo hicho kitafanyiwa marekebisho kitasaidia  kuondoa usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma  huku wauguzi wakiishi  mbali na sehemu yanakofanyia kazi.

“Ninafuraha kubwa na ni heshima kwangu kusaini mkataba wa mradi huu mpya kupitia mfuko wa mpango wa miradi midogo    kwa ajili ya usalama wa binadamu, hivyo basi tunatoa Sh bilioni 170 kwa ajili ya uboreshaji na ununuzi wa vifaa tiba.

“Tumepata taarifa wananchi wengi wanahudumiwa kwenye kituo hiki na wengine wanatoka mbali zaidi, naamini baada ya mradi huu kukamilika hudumu muhimu zitapatikana hapa na zitakuwa zinawasaidia wananchi wengi,” alisema Yoshida.

Alisema   Japan itaendelea kutoa michango yake katika kusaidia kituo hicho cha afya kusaidia upatikanaji wa  huduma mbambali.

Naye Profesa  Muhongo  alisema mradi huo utachukua mwaka mmoja kukamilika na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na imani naye ikiwa ni pamoja na kushirikiana ili aweze kutimiza  ahadi zake.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Anarose Nyamubi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk.Charles Mlingwa, alisema uboreshwaji wa kituo hicho utakuwa ni suluhisho katika kuboresha afya ya wananchi.

Alisema viongozi wengine wanapaswa kuiga mfano wa Profesa Muhongo kwa kufanya juhudi za kukutana na wadau mbalimbali katika kutaka kuwasaidia wananchi wanao waongoza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles