26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JAMII YAOMBWA KUWAKUMBUKA WAJANE

|Tunu Nassor, Dar es Salaam



Jamii imeombwa kujitolea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiwamo wajane na yatima ili nao waweze kuishi kwa furaha kama wengine.

Wito huo umetolewa na Mchungaji wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG),

Patrick Manda wakati kanisa hilo lilipokuwa likitoa msaada wa vyakula vikiwamo mchele, Unga wa sembe, sabuni, sukari na nguo vyenye thamani ya Sh milioni 2.2 kwa wajane 60 waliopo katika Mtaa wa Makongo Juu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo Mchungaji Manda amesema makundi hayo yamesahaulika na jamii na kuwafanya wahisi wametengwa.

“Tuna watu wengi wenye mahitaji kama hawa wanawake katika mitaa yetu hivyo natoa wito kwa taasisi za dini na jamii kwa ujumla kuwakumbuka kwa misaada ya mahitaji muhimu ya kibinadamu,” amesema Manda.

Kwa upande wao wajane hao wamelishukuru kanisa hilo kwa kuwakumbuka kwa kuwa wamekuwa wakipitia wakati mgumu kutokana na kutokuwa na watu wa kuwasaidia.

Mmoja wa wajane hao, Asha Said, amesema tangu amefiwa na mumewe mwaka 2002 hadi  jana hajawahi kusaidiwa na mtu yeyote wala kusikia kuna watu wanatoa misaada kwa wajane.

“Nilivyoambiwa kuwa kuna watu wanataka kutusaidia sikuamini kwa kuwa tangu nimefiwa nimekuwa nikihangaika bila msaada,” amesema Asha.

Naye kaimu Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Pius Prosper, amesema ni vyema kwa wengine kuiga mfano wa kanisa hilo kwa kuwa mtaa huo una yatima na wajane wengi ambao wanahitaji msaada wa kibinadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles