23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mutungi awaangukia Ukawa

Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Na Grace Shitundu, Dar es Salaam

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ameingilia kati kutafuta suluhu ya changamoto iliyojitokeza katika mchakato wa kutafuta katiba mpya.

Jaji Mutungi amefikia hatua hiyo na kukutana na viongozi wa vyama vya siasa pamoja na viongozi vya vyama waliounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao wamesusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.

Viongozi wa vyama vya siasa waliokutana na Jaji Mutungi ambao hata hivyo majina yao hayakutajwa walikuwa ni kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na NCCR Mageuzi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilisema Katika kikao hicho Jaji Mutungi aliwaeleza viongozi hao umuhimu wa kuendelea na mchakato wa kushiriki vikao vya Bunge maalumu pamoja na kuhakikisha yanakuwapo maridhiano baina yao.

“Kwa kuwa mimi ni mlezi wa vyama vya siasa na vyama hivyo vina nafasi kubwa katika mchakato huu niliona ni vizuri kuwaita kujadili na kushauriana jinsi ya kutatua changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha awali,” alisema.

Jaji Mutungi pia aliwataka viongozi hao kuweka maslahi ya Taifa mbele na  kuwataka wananchama wa vyama hivyo kuunga mkono juhudi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles