23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mahakama Kuu aahidi kuondoa changamoto mahakamani

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam



Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Atuganile Ngwala amesema atashirikiana na serikali kuhakikisha wanaondoa changamoto za kisheria zinazoikabili idara ya mahakama ili wananchi wapate haki zao.

Jaji Ngwala amesema hayo jana baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Uhakiki wa Mashauri ya Ardhi na Changamoto za Kisheria na Kitaasisi Tanzania Bara iliyotolewa jana na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete wakati wa Mahafali ya 48 ya yaliyofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema mahakama ni mhimili muhimu katika ustawi wa taifa, kwa sababu wananchi wamekuwa wakiwasilisha malalamiko yao ya kisheria ili waweze kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.

“Mahakama ni mhimili muhimu kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya pande zote mbili za walalamikaji na walalamikiwa ili waweze kupata haki zao, hivyo basi,  nitashirikiana na majaji wenzangu ili kuhakikisha tunafanya kazi kwa weledi na uadilifu na kutenda haki kwenye mashauri hayo kwa mujibu wa sheria,” amesema Jaji Ngwala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles