Imechapishwa: Mon, Oct 9th, 2017

JACKIE CHAN: SIRUDII FILAMU

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa filamu nchini China, Chan Kong-sang ‘Jackie Chan’, anatarajia kuachia filamu yake mpya ijulikanayo kwa jina la Rush 4 Hour, hivyo amesema hawezi kurudia kazi zake kwenye filamu nyingine.

Kwa sasa msanii huyo mwenye umri wa miaka 63, anafanya vizuri na filamu ya Rush 3 Hour, lakini amesisitiza filamu hiyo lazima iwe tofauti na inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

“Filamu hiyo mpya itakuwa ya kipekee, haiwezi kuzungumzia masuala ya dawa za kulevya, wala fedha bandia, hii itakuwa ya kipekee na tofauti sana. Siku zote sipendi kazi zangu kuzirudia kwenye filamu nyingine.

“Mashabiki wakae tayari kuona utofauti kati ya Rush 3 Hour na Rush 4 Hour, mbali na filamu hiyo kutakuwa na filamu nyingine kama vile Bleeding Steel na Viy 2: Journey to China,” alisema.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

JACKIE CHAN: SIRUDII FILAMU