28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

IS yamtangaza mrithi wa Baghdadi, yatoa onyo

BARISHA, SYRIA

KUNDI linalojiita Dola la Kiislamu IS limemtangaza kiongozi wake mpya baada ya kuthibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi katika shambulizi lililofanywa na Marekani nchini Syria.

Taarifa iliyotolewa kwenye chombo cha habari cha IS, al-Furqan imeeleza kuwa nafasi ya al-Baghdadi itazibwa na Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi.

Kundi la IS halikutoa taarifa zaidi kuhusu al-Qurayshi.

Kiongozi huyo mpya anatambuliwa kama msomi, shujaa mashuhuri na kiongozi wa kivita ambaye amepambana na majeshi ya Marekani na ana ufahamu kuhusu vita hivyo.

Taarifa hiyo pia imethibitisha kifo cha Abu Hassan al-Muhajir, msaidizi wa karibu wa al-Baghdadi ambaye alikuwa pia msemaji wa IS tangu mwaka 2016.

Vifo hivyo ni pigo kubwa kwa kundi la Dola la Kiislamu karibu miezi saba tangu lilipofurumushwa kutoka kwenye ngome yake ya mwisho nchini Syria.

Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la Kijihad la Islamic State (IS) na mtu ambaye alikuwa akisakwa sana duniani , alijiua kufuatia uvamizi wa Marekani uliotekelezwa na kikosi maalum cha wanajeshi kaskazini magharibi mwa Syria.

Kiongozi huyo aliyejiita ‘Khalifa Ibrahim’ alikuwa amewekewa dola milioni 25 kwa mtu yeyote ambaye angefichua maficho yake na alikuwa akisakwa na Marekani na washirika wake tangu kuanzishwa kwa kundi la IS miaka mitano iliopita.

Baghdadi aliapishwa kuwa kiongozi wa kundi hilo mwaka 2014 wakati ambao wanamgambo wa IS walipoweza kuishinda Iraq na Syria na kuanzisha utawala wao mpya wao.

Kutangazwa kwa mrithi huyo wa Baghidadi ambaye ni raia wa Saudi Arabia kunatajwa kuwa tishio jingine kwani anaelezwa kuwa ni ‘mrithi mzuri’.

Msemaji mpya wa IS, Abu Hamza al-Qurashi aliitwa pia ni msemaji mzuri wa al-Qurayshi.

Rais wa Marekani Donald Trump aliusifu uhuru huo wa Syria lakini akaongeza kuwa;  “Tutaendelea kuwa waangalifu dhidi ya IS”

Oktoba 22, mwaka huu, vikosi maalum vya Marekani vililenga nyumba mbili katika Mkoa wa Idlib na kabla ya kumkamata Baghidadi inaelezwa alijilipua mwenyewe.

Baghidadi ambaye alizaliwa mwaka 1971 alikuwa ni mzaliwa wa Samarra, nchini Iraq,  jina lake kamili ni Ibrahim Awad al-Badri.

Akiwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu tangu akiwa mdogo, baadaye mwaka 2004 alikuwa amefungwa katika kambi moja ya Marekani kwa jina Bucca kufuatia uvamizi wa Ufaransa na Marekani.

Akiwa katika kambi hiyo aliweka ushirikiano mzuri na wafungwa wengine wakiwemo maafisa wa zamani wa ujasusi nchini Iraq.

Alijifunza mengi kuhusu jinsi anavyoweza kufanya operesheni zake kutoka kwa maafisa wa kijasusi wa aliyekuwa rais wa Iraq, Sadaam Hussein.

Usalama wake ulikuwa ni wa hali ya juu ,kutokana na kiwango cha juu cha wasiwasi alionao.

Alikiri kuhusu kushindwa kwa kundi lake na kusema kwamba IS ilikuwa ikipigana vita vya kupunguza nguvu za adui, akiwataka wafuasi wake kutekeleza mashambulio yatakayowaondoa wapinzani wao, kupitia wanadamu, kijeshi, kiuchumi, na raslimali za kimkakati.

Kabla ya kifo chake Baghidadi aliwahi kuzungumza kupitia kanda ya video ambayo haikubainika ilikorekodiwa na alionekana kuwa buheri wa afya.

Alionekana akiwa ameketi na takriban watu watatu ambao nyuso zao zilikua zimefichwa.

Pia aliwataka wafuasi kuwaaachilia huru maelfu ya washukiwa wa IS na maelfu ya wanawake na watoto wanaohusishwa na IS ambao walikuwa wakizuiliwa katika jela za SDF na kambi za Syria kufuatia kukombolewa kwa Baghuz.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles