33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Iran yaendelea na msimamo wake utengenezaji makombora

TEHRAN, IRAN

RAIS Hassan Rouhani amesisitiza kwamba Serikali yake itaendelea kutengeneza makombora ya aina mbalimbali bila ya hofu na katu hailazimiki kumwomba idhini mtu ywyote kutekeleza azma yake hiyo.

Wairan wako kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 ya mapinduzi ya Kiislamu yaliyouangusha utawala wa Shah Mohammed Reza Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Ujumbe mkubwa uliotolewa na Rais Rouhani umesisitiza kwamba Iran haitompigia mtu yeyote magoti au kuomba ridhaa yake kuendelea na harakati zake za kujiimarisha kijeshi.

Hotuba ya Rais Rouhani imetilia mkazo kwamba njama zinazofanywa na adui dhidi ya Iran zitashindwa kwa namna zote na kuonya kwamba sasa Jamhuri hiyo ya Kislamu ina nguvu kubwa zaidi kuliko wakati ilipopambana na Saddam Hussein wa Irak katika vita vilivyosababisha maafa makubwa na uharibifu kutoka mwaka 1980 hadi 1988.

Rais Rouhani alisema leo hii ulimwengu unapaswa kutambua kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo mkubwa zaidi kuliko siku za vita na huku akiipuuzia   miito kutoka Marekani na Ulaya ya kutaka pafanyike makubalino mapya ya kuuzuia mpango wake wa nyuklia.

“Mwaka huu tunasherehekea miaka 40 ya kinachoangaliwa kama siku ya ushindi katika mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 ya nchi yetu dhidi ya njama za wahalifu Wamarekani, Wazayuni na nchi zilizopitwa na wakati za kanda hii ambazo zinataka kuwaangusha watu wetu kupitia shinikizo na vikwazo.

“Leo uwepo wa umma mitaani katika sherehe hizi za kumbukumbu kote nchini kunamaanisha kwamba njama za maadui zimeshindwa. Uwepo huu unamaanisha kwamba adui hatofanikiwa katika malengo yake ya uovu,” alisema Rais Rouhani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles