27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Iran waanza kampeni za uchaguzi wa bunge kwa vikumbo

Tehran, Iran    

MAELFU ya wagombea walioidhinishwa kushiriki katika uchaguzi wa bunge nchini Iran wameanza kampeni zao jana kabla ya kufanyika uchaguzi huo wa wiki ijayo.

Aidha maofisa wameonekana kuwazuia maelfu kugombea, wengi wao wakiwa wanamageuzi na viongozi wa siasa za wastani.

Uchaguzi huo wa bunge wa Februari 21 unakuja wakati kukiwa na mvutano mkubwa kabisa kati ya Iran na Marekani kuwahi kushuhudiwa katika miongo minne.

Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameshutumu hatua ya kuzuiwa wagombea hao lakini mapema wiki hii, akawaomba wafuasi wake mjini Tehran wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya mwaka wa 1979 wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupigia kura.

Kura hiyo inaonekana kuupima umaarufu wa kundi la siasa za wastani na za kimaendeleo linaloongozwa na Rouhani, ambaye amepata changamoto katika kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za kuimarisha maisha ya watu wakati Iran ikikabiliwa na vikwazo vikali vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles